TANZANIA YAVUNJA REKODI TUZO ZA KIMATAIFA ZA DSTV EUTELSAT STAR!

  Tanzania yavunja rikodi Tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star! Rasheed Taher aiingiza Tanzania kwenye nchi zilizowahi kuwa wash...



 
Tanzania yavunja rikodi Tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star!


Rasheed Taher aiingiza Tanzania kwenye nchi zilizowahi kuwa washindi


Kampala, Paris, 13 April 2018 – Tanzania imevunja rekodi kwenye Tuzo za kimataifa za wanafuzi zijulikanazo kama DStv Eutelsat Star Awards baada ya  mwanafunzi Taher Rasheed kutoka shule ya Al-Madrasat Us-saifiyatul Burhaniyah ya Dar es salaam kushinda nafasi ya kwanza katika category ya poster(bango) baada ya mchuano mkali na mamia ya wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Kwa upande wa insha mshindi alikuwa Amos Mumbere kutoka shule ya Ntare nchini Uganda


Tuzo hizi ambazo zinahusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango vyenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait ni za wazi kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19 kote barani Afrika ambapo kampuni ya MultiChoice inaendesha shughuli zake.


Mwaka huu, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango kuhusu manufaa yaliyoletwa na uvumbuzi wa setelaiti katika maisha ya kila siku hapa ulimwenguni na ni jinsi gani setelait imekuwa kama kiungo muhimu kwa shughuli zote zinazofanyika kote duniani.
Taher alitangazwa rasmi jana jioni jijini Kampala nchini Uganda ambapo jopo la watahini maarufu lilikaa na kupitia kazi za wanafunzi kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Jopo hilo liliongozwa na Paolo Nespoli, mwanaanga nguli kutoka European Space Agency (ESA).


Akiongea baada ya kupokea habari hizo za ushindi, Taher amesema amefurahi sana kwa ushindi huo mkubwa ambao umemletea yeye, shule yake na taifa zima kwa ujumla sifa kubwa. “Nimefurahi sana kupokea taarifa hizi nzuri. Naamini ushindi wangu utakuwa ni chachu kubwa kwa wanafunzi wenzangu kote nchini kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika tuzo kama hizi na mashindano mengine ya kitaaluma ya ndani na nje ya nchi” alisema Taher.


Naye mkurugenzi mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande amesema wamefurahishwa sana na ushindi huo wa Tanzania katika mashindano hayo muhimu ya kitaaluma ya kimataifa. Amesema kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa pamoja na MultiChoice Afrika na kituo cha anga cha Eutelsat huko Ufaransa kwa madhumuni makubwa ya kuwajengea wanafunzi ari ya kushiriki katika masomo ya sayansi na pia kuhamasisha ubunifu na ugunduzi katika tasnia ya sayansi.


Ameongeza kuwa kwa ushindi huu ni dhahiri kuwa wanafunzi wa Tanzania wana uwezo mkubwa wa kushiriki na kushindana katika yanja ya taaluma ya sayansi na pia inadhihirisha kuwa vijana wetu wana uwezo mkubwa hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa vipaji hivi vinakuzwa na kuendelezwa kwa manufaa ya taifa letu” alisema Maharage.


Mshindi wa bango atajishindia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini na kutembelea kituo cha anga cha nchi hiyo na pia makao makuu ya MultiChoice Africa akiwa kama mgeni maalum.  Shule zitakazotoa washindi hao zitapata zawadi ya kufungia huduma ya DStv bure.


About Eutelsat
Founded in 1977, Eutelsat Communications is one of the world's leading satellite operators. With a global fleet of satellites and associated ground infrastructure, Eutelsat enables clients across Video, Data, Government, Fixed and Mobile Broadband markets to communicate effectively to their customers, irrespective of their location. Over 6,700 television channels operated by leading media groups are broadcast by Eutelsat to one billion viewers equipped for DTH reception or connected to terrestrial networks. Headquartered in Paris, with offices and teleports around the globe, Eutelsat assembles 1,000 men and women from 32 countries who are dedicated to delivering the highest quality of service.
For more about Eutelsat go to www.eutelsat.com
About MultiChoice Africa
Entertainment is a powerful way to tell stories that open our minds, bring people together around shared passions, and connect us to new realities. It makes us laugh and cry. It informs, it educates and it inspires. MultiChoice is a video entertainment company, and our purpose is to enrich lives. We make the best in entertainment accessible to millions of households in 49 countries across Sub-Saharan Africa. We do this through cutting-edge technology on our DStv and GOtv platforms – delivering the content our customers love and contributing to the success of local economies. Born and bred in Africa, we are rooted in the countries where our customers live. We are managed and run by local people, and strive to provide all our employees with new opportunities. We’re proud of the contribution we make to our communities, and our business has grown hand-in-hand with local economies by forging long-term partnerships with governments, national broadcasters and entrepreneurs. We want to use our

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANZANIA YAVUNJA REKODI TUZO ZA KIMATAIFA ZA DSTV EUTELSAT STAR!
TANZANIA YAVUNJA REKODI TUZO ZA KIMATAIFA ZA DSTV EUTELSAT STAR!
https://lh6.googleusercontent.com/gtjjbHx4RBLIHlj5O2BjsC7HgbQrgDH7b4L5-qTu438KjAjcFaa2zABx7U3udi8u4NdMMQvuvu-Z10E99W5w7KptkNmuExnXVRYlkZWYOMi6w_oWduxbavYTKj8R90l65CwxTXnnIjb4Q-KAMQ
https://lh6.googleusercontent.com/gtjjbHx4RBLIHlj5O2BjsC7HgbQrgDH7b4L5-qTu438KjAjcFaa2zABx7U3udi8u4NdMMQvuvu-Z10E99W5w7KptkNmuExnXVRYlkZWYOMi6w_oWduxbavYTKj8R90l65CwxTXnnIjb4Q-KAMQ=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/tanzania-yavunja-rekodi-tuzo-za.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/tanzania-yavunja-rekodi-tuzo-za.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy