SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla fupi ya makabidhia...



Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw Festo Kiswaga (kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa( TANAPA) Allan Kjazi akikabidhi Hundi ya Kiasi cha Sh Mil 50 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa huo ,wengine kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete na Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Bw Festo  Kiswaga (kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Anthony Mtaka akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za TAifa (TANAPA) Pascal Shelutete mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa wa Simiyu.

(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini)



Shirika la Hifadhi za Taifa leo limekabidhi mchango wa
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tatu za vipaji maalumu katika mkoa wa Simiyu za Simiyu Ufundi, Simiyu Wavulana na Simiyu Wasichana


Mchango huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.
Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya
sekondari ya ufundi mkoani Simiyu ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya mkoa katika kuimarisha sekta ya elimu ambapo pia mkoa umepanga kuje nga shule nyingine maalum mbili za sekondari za  wasichana na
wavulana.

 Kwa pamoja Mhe Mtaka aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga waliahidi kuzitumia fedha hizo kama zilivyokusudiwa na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umuhimu wa wananchi kuheshimu sekta ya uhifadhi kwa kuwa ina manufaamakubwa kwao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi
aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wana Simiyu kwa kuwa mkoa huo umekuwa mstari wa mbele katika kusimamia sheria za hifadhi hususan Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuzuia uingizaji wa mifugo pamoja na majangili.

Shule ya Ufundi ya Simiyu inatarajiwa kugharimu kiasi cha
Shilingi Milioni 350 hadi itakapokamilika na wadau mbalimbali wameombwa kuunga mkono jitihada hizo za Simiyu.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU
SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiWkPCk8bu8m3yHMuoIUm0QmoW0wdToSGRgHh97k700dT_PzQmVfwHGtqkn_HIbfhAEWszAEWs5e7lsn7vJFl8_EoUCxJyXHt9hV6FvH1k9vFXEiIaJ1j4xo0YWv07jteg0tqaayu_cTtTT/s640/5.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiWkPCk8bu8m3yHMuoIUm0QmoW0wdToSGRgHh97k700dT_PzQmVfwHGtqkn_HIbfhAEWszAEWs5e7lsn7vJFl8_EoUCxJyXHt9hV6FvH1k9vFXEiIaJ1j4xo0YWv07jteg0tqaayu_cTtTT/s72-c/5.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/shirika-la-hifadhi-za-taifa-tanapa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/shirika-la-hifadhi-za-taifa-tanapa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy