SERIKALI YAWAREJESHA KAZINI WATUMISHI WA DARASA LA SABA WALIOKUWA KAZINI KABLA YA MEI 20, 2004
HomeJamii

SERIKALI YAWAREJESHA KAZINI WATUMISHI WA DARASA LA SABA WALIOKUWA KAZINI KABLA YA MEI 20, 2004

NA LILIAN LUNDO - MAELEZO, DODOMA. SERIKALI imeamuru kurudishwa kazini kwa Watumishi wote ambao walikuwa na ajira za kudumu au ajira za mik...

WADAU WA MAENDELEO WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF.
TANZANIA KUUNGANA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA MATAIFA KUADHIMISHA SIKU YA MARALIA DUNIANI 2018
SPIKA EALA AIPONGEZA TANZANIA KWA MAENDELEO


NA LILIAN LUNDO - MAELEZO, DODOMA.

SERIKALI imeamuru kurudishwa kazini kwa Watumishi wote ambao walikuwa na ajira za kudumu au ajira za mikataba (kwa watendaji wa Vijiji na Mitaa) au ajira za muda ambao walikuwa kazini kabla ya Mei 20, 2004 ulipoanza kutumika waraka wa Utumishi Na. 1 wa mwaka 2004 ambao umetaja kuwa cheti cha ufaulu wa mtihanai wa kidato cha nne kama sifa ya msingi kwa mtumishi wa Umma.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika alipokuwa akitoa Kauli ya serikali kuhusu watumishi waliondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mshahara kwa kukosa sifa ya cheti cha kufaulu mtihani wa elimu ya kidato cha nne.

"Watumishi wa Umma Elfu Moja Mia Tatu Sabini (1,370) waliolegezewa masharti ya sifa za muundo kupitia barua ya Katibu Mkuu Utumishi yenye Kumb. Na. CCB.271/431/01/p/13 ya tarehe 30 Juni, 2011 warejeshwe kazini mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa Sheria," alisema Mhe. Mkuchika.

Hata hivyo amesema kuwa uamuzi huu uliotajwa hautawahusu watumishi wawasilisha vyeti vya kughushi katika kumbukumbu za ajira zao, watumishi waliokuwepo katika ajira kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 pamoja na warumishi wote walioajiriwa baada ya tarehe 20 Mei 2004 wakiwa hawana sifa za kufaulu mtihani wa kidato cha nne kwa kuwa walijipatia ajira kinyume cha maelekezo ya Serikali.

Aidha, watendaji wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi wote walioshiriki kuwaajiri Watumishi wasiokuwa na sifa ya kufaulu mtihani wa kidato cha nne katika Utumishi wa Umma baada ya tarehe 20 Mei, 2004 watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria, kanuni za taratibu.

Vilevile watendaji wakuu na maafisa wote wanaosimamia zoezi hili ambao kwa namna yoyote ile watashiriki kuhujumu zoezi hili kwa kuondoa au kuharibu kumbukumbu za Watumishi ili haki isitendeke, watachukuliwa hatua za kinidhamu na za kijinai ikibidi.
















Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YAWAREJESHA KAZINI WATUMISHI WA DARASA LA SABA WALIOKUWA KAZINI KABLA YA MEI 20, 2004
SERIKALI YAWAREJESHA KAZINI WATUMISHI WA DARASA LA SABA WALIOKUWA KAZINI KABLA YA MEI 20, 2004
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZKuxnqjlo9poujQZixMJG7B4_DzqBcwQv0_jPtlUIeH5kwl9GkrUbtl6iAKaQthMouChJ0mgTxIdejdni6tjkYbdObd2P8CajIWCbg-2OHxgB0QnldrwZf8p0wNrEa3OTQeWSSI5wB5c/s320/mkuchika.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZKuxnqjlo9poujQZixMJG7B4_DzqBcwQv0_jPtlUIeH5kwl9GkrUbtl6iAKaQthMouChJ0mgTxIdejdni6tjkYbdObd2P8CajIWCbg-2OHxgB0QnldrwZf8p0wNrEa3OTQeWSSI5wB5c/s72-c/mkuchika.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/serikali-yawarejesha-kazini-watumishi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/serikali-yawarejesha-kazini-watumishi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy