MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema leo Aprili 10, 2018 kuwa kati ya wanawake 480 waliofanikiwa kuonana na timu yake ya...

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema leo Aprili 10, 2018 kuwa kati ya wanawake 480 waliofanikiwa kuonana na timu yake ya wanasheria na maafisa wa ustawi wa jamii, 47 wamewataja wabunge waliowazalisha na kuwatelekeza huku 14 wakiwataja viongozi wa dini kuwa ndio wahusika.
Mhe. Makonda amewaalika wanawake jijini Dar es Salaam, ambao wametekelezwa na wanaume waliozaa nao na kwamba wasiwe na hofu kwani “mbivu mbichi” zitabainika na kila mtu ataondoka na haki yake.
Zaidi ya wanawake 1,000 waliweka kambi ofisini kwa mkuu wa mkoa ili kupatiwa msaada huo wa kisheria na ushauri ambapo wengi wao walifika wakiwa na ushshidi “watoto” na kumsifu Mkuu wa Mkoa wa kwa hatua hiyo kwani walisubiri sana kuona wanapatiwa masaada baada ya kutelekezwa.
Miongoni mwa wanawake waliotelekezwa na watoto ni pamoja na Yule aliyezaa na mfanyakazi wa kichina ambaye kwa sasa hayupo nchini.

COMMENTS