RC MAKONDA KUKUTANA NA KAMPUNI 30 KUTOKA UFARANSA, AWASHAURI WAFANYABISHARA DAR KUCHANGAMKIA FURSA
HomeJamii

RC MAKONDA KUKUTANA NA KAMPUNI 30 KUTOKA UFARANSA, AWASHAURI WAFANYABISHARA DAR KUCHANGAMKIA FURSA

Na Bakari Madjeshi, Globu ya jamii MKUU wa mkoa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini, Federic Clavier ambapo kw...

GOVERNMENT LAUNCHES 'NIPO TAYARI' CAMPAIGN
TANESCO YAWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA MAPEMA WAONAPO HITILAFU YA UMEME ILIYOSABABISHWA NA MVUA AUKITU KINGINE
SERIKALI KUCHIMBA MABWAWA YA MAJI ILI KUPUNGUZA UHABA WA MAJI NCHINI

Na Bakari Madjeshi, Globu ya jamii

MKUU wa mkoa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini, Federic Clavier ambapo kwa sehemu kubwa mazungumzo yao yamejikita kujadili kuhusu kongamano la uchumi litakalofanyika mapema jumatatu wiki ijayo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Makonda amemshukuru balozi na kueleza kuwa wamekuwa marafiki wazuri na Serikali ya Tanzania.Kuhusu kongamano hilo Makonda amesema siku ya Jumatatu Kampuni 30 kutoka Ufaransa yatawasili nchini na kufanya mkutano wenye malengo ya kuufanya mji wa Dar es salaam kuwa kama miji mingine duniani katika masuala ya maji, afya, usafiri na masuala mengine ya kiteknolojia.

Aidha ameeleza kampuni hizo zitaangalia fursa na vipaumbele vya Serikali watakavyovitumia katika kuleta maendeleo na ametoa rai kwa wafanyabiashara wa Jiji la Dar es salaam kuja katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kujifunza na kuunganishwa na wafanyabiashara hao kutoka ufarasa ili waweze kujifunza na kujenga urafiki katika masoko ya bidhaa zao.

Kwa upande wa Balozi wa Ufaransa nchini Federic Clavier amefurahi na kumshukuru Mkuu ya Mkoa Dar na kueleza kuwa Dar es Salaam ni mji unaoendelea kukua kiuchumi sambamba na dhamira ya Rais Dk. John Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025. Aidha amesema mkutano huo utakuwa na faida baina ya nchi hizi mbili hasa katika kubadilishana teknolojia katika sekta mbalimbali hasa kwa kuangalia afya, maji pamoja na miundombinu na amehaidi matokeo mazuri yenye faida kwa nchi hizo.

Kuhusu mchakato wa kusaidia watoto waliotelekezwa Makonda amewashukuru wanahabari kwa kuwa sehemu ya wapatanishi wa familia hizo aidha amewataka wananchi kuja kupata huduma katika viwanja vya ofisi yake na si katika simu na mitandao na amefafanua hadi sasa familia 178 wameelewana na kukubaliana kupeana fedha za matunzo na zaidi ya watu 1498 wameshapatiwa huduma.

"Na Jumatatu wataitwa baba wa familia hizo licha ya baadhi yao kuanza kuripoti na ameeleza kuwa walio tayari kupima DNA wajitokeze watakaokaidi watachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkaribisha Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier mapema leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
(Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RC MAKONDA KUKUTANA NA KAMPUNI 30 KUTOKA UFARANSA, AWASHAURI WAFANYABISHARA DAR KUCHANGAMKIA FURSA
RC MAKONDA KUKUTANA NA KAMPUNI 30 KUTOKA UFARANSA, AWASHAURI WAFANYABISHARA DAR KUCHANGAMKIA FURSA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwLu9V3nf8DjJCnFa4y2hPQSCW9-kS6uV3nv9aQE4KZDmzIXMGYvBxbLBh3sjWuTRc5UN5lZR2s3W557FzCqBiva9PPk3hgK7c1Tok7BB2NNjcZ8EZUtKXq1N9ICN3J4dchztztXaQiQjD/s640/11.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwLu9V3nf8DjJCnFa4y2hPQSCW9-kS6uV3nv9aQE4KZDmzIXMGYvBxbLBh3sjWuTRc5UN5lZR2s3W557FzCqBiva9PPk3hgK7c1Tok7BB2NNjcZ8EZUtKXq1N9ICN3J4dchztztXaQiQjD/s72-c/11.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/rc-makonda-kukutana-na-kampuni-30.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/rc-makonda-kukutana-na-kampuni-30.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy