Na Husna Saidi. SERIKALI imesema imeandaa mpango kabambe wa uchimbaji wa mabwawa ya kutiririsha maji ya mvua katika baadhi y...
Na Husna Saidi.
SERIKALI
imesema imeandaa mpango kabambe wa uchimbaji wa mabwawa ya kutiririsha
maji ya mvua katika baadhi ya maeneo nchini ili kupunguza hadha ya
ukosefu wa maji kwa wananchi.
Hayo
yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo na Wazirti katika kikao
cha Bunge la bajeti linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu Majaliwa alisema katika kutekekeleza mpango wa Serikali kumtua
“Mama ndoo kichwani” Serikali imedhamiria kupunguza umbali mrefu
wanaotumia wananchi kutafuta maji, ambapo imepanga kuchimba mabwawa
makubwa ya maji katika maeneo ambayo yana mtiririko wa maji.
“Tutaendelea
kutoa maelekezo kwa Watendaji wetu kuhamasisha wananchi kutumia fursa
ya misimu wa mvua ili kujiwekea akiba ya maji ambayo yatawasaidia wakati
wa kipindi cha kiangazi hususani katika maeneo ambayo yana uhaba wa
maji”.
Kwa
mujibu wa Majaliwa alisema katika Bajeti ya Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Serikali imeandaa mpango maalum wa uchimbaji wa mabwawa ya
maji sambamba na kufanya ukarabati wa mabwawa ambayo yameharibiwa na
mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Aidha
Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka Halamashauri zote nchini kuhakikisha
zinatumika vyema mabwawa na mifereji iliyokuwa katika maeneo ili kuweza
kuvuna maji ya mvua na kuyahifadhi kwa msimu huu wa mvua na ujao.
Majaliwa
aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya
kukarabati miundombinu ya mabwawa yote nchini ili kuhakikisha
halmashauri zote nchini zinakuwa na utoshelevu wa huduma ya maji kwa
wananchi wake.
Waziri
Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali Mbalimbali ya Wabunge katika
kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini
Dodoma Mei 11, 2017.
COMMENTS