TANESCO YAWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA MAPEMA WAONAPO HITILAFU YA UMEME ILIYOSABABISHWA NA MVUA AUKITU KINGINE
HomeJamii

TANESCO YAWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA MAPEMA WAONAPO HITILAFU YA UMEME ILIYOSABABISHWA NA MVUA AUKITU KINGINE

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limewaomba wateja wake na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa map...

CLOUDS TV YAPEWA TUZO YA KITUO BORA CHA TELEVISHENI 2017
WADAU WATAKIWA KUJITOKEZA KUFADHILI TAMASHA LA WATOTO CHRISMASS
TAARIFA KUHUSU UINGIZWAJI WA MIFUGO NCHINI TANZANIA




NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limewaomba wateja wake na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa mapema mara inapotokea hitilafu ya umeme iliyosababishwa na mvua au sababu nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2017, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, sambamba na hilo pia wananchi wasifanye shughuli au kukaa chini ya miundombinu ya umeme.
“Lakini tunawaomba wananchi watoe taarifa haraka maeneo yenye mafuriko au mkusasnyiko wa maji mengi ili wataalamu wetu waweze kuchukua hatua za haraka.” Alisema.
Dkt. Mwinuka pia alisema endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha umeme kimepata hitilafu na kinahatarisha maisha ni vema uangalizi au alama ikawekwa ili kuwapa hadhari wapiti njia na watoto wasikaribie eneo hilo wakati mafundi wa TANESCO wakichukua hatua za marekebisho.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), katika taarifa yake iliyotoa Mei 9, 2017 imeonya kuwa maeneo ya Pwani ya Kaskazini ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba, yatakabiliwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kuanzia Mei 10 hadi 12, 2017. Aidha kwa upande wake, mtaalamu wa masualaya umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Simon Kihiyo, amewahakikishia wananchi kuwa miundombinu ya TANESCO iko imara na salama, na hitilafu  zinazotokea za hapa na pale nyingizinasababishwa na sababu za kibinadamu, au za kimazingira kama vile nguzo za umeme kugongwa na magari, au miti kuangukia nguzo. "Naomba nitoe angalizo kwa wateja wetu, kama pametokea hitilafu yoyote ya umeem nyumbani kwako, ni vema ukatoa taarifa TANESCO au ukamtafuta fundi wa umeme mwenye taaluma badala ya kushughulikia tatizo hilo wewe mwenyewe ilihali ukiwa huna utaalamu na masuala ya umeme, kwani hiyo ni hatari."
Naye kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji amesema, katika kipindi hiki cha mvua kuna athari ndogo ndogo zimetokea kwenye miundombinu ya TANESCO hususan nguzo za umeme, lakini akatoa hakikisho kuwa mafundi wa TANESCO wanekuwa wakichukua hatua za haraka kurekebisha athari katika miundombinu ya umeme pindi tu zinapotokea.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Me11, 2017. Dkt. Mwinuka ametoa hadhari kwa wananchi kutogusan miundombinu ya Tanesco hususan nyaya zilizoanguka, au kufanya shughuli yoyote karibu na miundombinu yab umeme katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendela kunyesha nchini. Kulia ni Mhandisi Simon Kihiyo, na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.

 Mhandisi Simon Kihiyo, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu hatua za kuchukua pindi hitilafu ya umeme inapotokea
 Dkt. Mwinuka (kushoto) na MhandisiKihiyo, wakati wa mkutano huo leo
 Dkt. Mwinuka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
 Waandishi wa habari wakiwa kazini
  Waandishi wa habari wakiwa kazini
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, akitoaufafanuzi zaidi wa hatua za kuchukua endapo wateja au wananchi wataona hitlafu ya umeme kwenye maeneo yanayowazunguka
 Mhandisi Kihiyo, (kulia0na Kaimu Meneja Uhusianowa TANESCO Leila Muhaji katika mkutano na wanahabari
Mhandisi Simon Kihiyo, (kulia), Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (kushoto) na Afisa Uhsiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila wakijadiliana jambo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANESCO YAWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA MAPEMA WAONAPO HITILAFU YA UMEME ILIYOSABABISHWA NA MVUA AUKITU KINGINE
TANESCO YAWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA MAPEMA WAONAPO HITILAFU YA UMEME ILIYOSABABISHWA NA MVUA AUKITU KINGINE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpJiqfb85ExPQKAZEuUbBmaeyh2xOa51mme9b9THFIGukWCiQdO4xvoFIwk4qtZb-UCmyf9RTKgp1R-d_v5DFWB61s2PIZybS_zMggs8AshuSksCf3ay2fuusTaQP91Y9tQTP0DejYi6o/s640/5R5A1537.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpJiqfb85ExPQKAZEuUbBmaeyh2xOa51mme9b9THFIGukWCiQdO4xvoFIwk4qtZb-UCmyf9RTKgp1R-d_v5DFWB61s2PIZybS_zMggs8AshuSksCf3ay2fuusTaQP91Y9tQTP0DejYi6o/s72-c/5R5A1537.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tanesco-yawaomba-wananchi-kutoa-taarifa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tanesco-yawaomba-wananchi-kutoa-taarifa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy