RAIS MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA UMEME WA MW 240 WA KINYEREZI II JIJINI DAR ES SALAAM, AIPONGEZA TANESCO KWA UTENDAJI MZURI
HomeJamii

RAIS MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA UMEME WA MW 240 WA KINYEREZI II JIJINI DAR ES SALAAM, AIPONGEZA TANESCO KWA UTENDAJI MZURI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz To...

MICHANGO NA MAFAO YA WANACHAMA KATIKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII IKO SALAMA
UFARANSA YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUPAMBANA NA RUSHWA
MDAHALO WAKUWANIA UONGOZI WA URAIS JUMUIYA YA WATANZANIA DMV
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Aprili, 2018 amezindua mradi wa kuzalisha megawati 240 za umeme kwa kutumia gesi asilia (Kinyerezi II) uliopo Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kuzindua mradi huo Mhe. Rais Magufuli amekagua mitambo 6 ya kisasa inayotumia teknolojia mpya na ya kwanza kufungwa Afrika Mashariki iitwayo “Combined Cycle” ambayo inatumia hatua mbili za kuzalisha umeme kwa kutumia gesi na mvuke.
Teknolojia hii itaiwezesha mitambo ya Kinyerezi II kuzalisha megawati 167.82 kwa kutumia gesi asilia na megawati 80.4 kwa kutumia mvuke na mpaka sasa tayari megawati 160 zimeshaanza kuzalishwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa, megawati 40.2 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwezi Mei na megawati 48 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka amesema mradi huu umegharimu Shilingi Bilioni 798, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania ambapo kati ya fedha hizo asilimia 15 zimetolewa fedha taslimu na asilimia 85 zimekopwa kutoka benki za Japan.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Matogolo Kalemani amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa jitihada zake za kuimarisha upatikanaji wa umeme hapa nchini ikiwemo kuhakikisha mradi wa uzalishaji wa umeme wa Kinyerezi II unakamilika, upanuzi wa Kinyerezi I kwa kuongeza uzalishaji umeme kutoka megawati 150 hadi kufikia megawati 335 na kutekeleza mradi wa uzalishaji wa umeme megawati 2,100 katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers Gorge) ambayo ikikamilika itaiwezesha nchi kuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 5,000 za umeme.
Dkt. Kalemani amebainisha kuwa pamoja na kutekeleza miradi hiyo Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza miradi ya usafirishaji na usambazaji wa umeme mkubwa ya Iringa – Dodoma – Singida – Shinyanga (kilovoti 400, kilometa 679), Singida – Arusha – Namanga (kilovoti 400, kilometa 414), Makambako – Songea (kilovoti 220, kilometa 300) na mradi wa umeme vijijini (REA) umevifikia vijiji vipya 4,916 na wateja wapya 874,984.
Katika hotuba yake Mhe. Rais Magufuli ameipongeza TANESCO kwa kazi nzuri inayoifanya na amempongeza mkandarasi kampuni ya Sumitomo Corporation kwa kukamilisha mradi wa Kinyerezi II siku 45 kabla ya muda uliopangwa na kuwaajiri Watanzania kwa asilimia 80 ya wafanyakazi wote 2,000 waliopata ajira katika mradi huo.
Mhe. Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Nishati kuongeza juhudi za kusambaza umeme kwa wananchi ili kuepuka madhara yakiwemo uharibifu wa misitu unaosababisha hekta 400,000 kufyekwa kila mwaka kwa ajili ya kuni na mkaa.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa wizara, idara na taasisi za Serikali kuwasiliana pale kunapokuwa na changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo vifaa kukwama bandarini kutokana na kudaiwa kodi ili kuepusha ucheleweshaji na ongezeko kubwa la gharama za miradi hiyo.
Mhe. Rais Magufuli amewaondoa shaka wananchi wa Dar es Salaam kuwa japo Serikali inahamia Dodoma Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuboreshwa na ameitaja baadhi ya miradi kuwa ni ujenzi wa barabara za juu (Flyover), ujenzi wa uwanja wa ndege (Terminal 3), reli ya kisasa (Standard Gauge), bandari, barabara na mradi wa kujenga vizuri eneo la bonde la Msimbazi.
“Hatutalitelekeza Jiji la Dar es Salaam, ninachowaomba endeleeni kuungana na Serikali katika juhudi hizi  za maendeleo na msikubali watu wawashawishi kuvuruga amani kwa kuwa nchi hii ni yetu sote” amesema Mhe. Rais Magufuli.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Aprili, 2018




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiboneza kitufe kuashiria kuwasha rasmi mtambo wa Umeme wa kinyerezi II nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, leo Aprili 3,2018, na kuimwagia sifa TANESCO kwa akzi nzuri wanayoendelea kuifanya katika sekta ya umeme nchini. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Dkt. Medard Kalemani Waziri wa Nishati akitoa maelekezo kuhusu mitambo ya kufua umeme kabla ya kuzindua rasmi mtambo wa kinyerezi II nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Aprili 3,2018.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi II Mhandisi Stivin Manda akitoa maelekezo kuhusu mradi wa kufua umeme kabla ya kuzindua rasmi mtambo wa kinyerezi II nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.Aprili 3,2018.


Mtambo mpya wa umeme wa Kinyerezi II uliozinduliwa rasmi na Mhe. Rais leo.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mitambo ya kufua umeme kabla ya kuzindua rasmi mtambo wa kinyerezi II nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.Aprili 3,2018.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwakilishi wa Balozi wa Japan Nchini Bw. Hiloyuki Kubota wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi mtambo wa umeme wa kinyerezi II nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.Aprili 3,2018.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhe.Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi mtambo wa umeme wa kinyerezi II nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Aprili 3,2018.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wa kuwaaga wananchi waliohuduria katika sherehe za uzinduzi rasmi mtambo wa umeme wa kinyerezi II nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Aprili 3,2018. (PICHA NA IKULU)


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA UMEME WA MW 240 WA KINYEREZI II JIJINI DAR ES SALAAM, AIPONGEZA TANESCO KWA UTENDAJI MZURI
RAIS MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA UMEME WA MW 240 WA KINYEREZI II JIJINI DAR ES SALAAM, AIPONGEZA TANESCO KWA UTENDAJI MZURI
https://lh6.googleusercontent.com/Fmn2mohATycTT7LEKUcFLhFY80sk87uVfHlOvNSR9LpOVq8gsdR6xhRUvatgxxQm8SnTf4tTtuaAuFTixIEUevZokmQQLt3NaQXpC6CDkkYaKAlMLVzbJbpgX_gyLD3YXSuoWxwLRy_4VbsQWQ
https://lh6.googleusercontent.com/Fmn2mohATycTT7LEKUcFLhFY80sk87uVfHlOvNSR9LpOVq8gsdR6xhRUvatgxxQm8SnTf4tTtuaAuFTixIEUevZokmQQLt3NaQXpC6CDkkYaKAlMLVzbJbpgX_gyLD3YXSuoWxwLRy_4VbsQWQ=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/rais-magufuli-azindua-rasmi-mradi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/rais-magufuli-azindua-rasmi-mradi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy