RAIS DKT MAGUFULI, EAC TUNAWEZA KUJITEGEMEA.
HomeJamii

RAIS DKT MAGUFULI, EAC TUNAWEZA KUJITEGEMEA.

Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wanaafrika Mashariki kuji...

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA JUMAPILI KANISA KUU LA MT. PAULO WA MSALABA MJINI DODOMA
TANROADS WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA
WAHITIMU TIA WAMEASWA KUJIHUSISHA NA UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA NA RUSHWA



Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wanaafrika Mashariki kujiamini kuwa wanaweza kutekeleza miradi ya maendeleo bila kutegemea mataifa mengine.
Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa  akihutubia Bunge la Nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofanyika mkoani humo kwa mara kwanza  tangu kuanza kwa Bunge hilo.
“Ninazungumza hili si kwamba hatuhitaji msaada au hatuhitaji ushirikiano, lakini ni lazima tuliweke hili wazi, kwamba tukiamua tunaweza na mifano ipo mingi ikiwemo Tanzania”. Alisisitiza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.
“Tanzania tunajenga reli ya kisasa yenye urefu wa kilometa 700.26 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa thamani ya shilingi Trilioni 7.6, tumeweza kununua ndege sita na pia tumejenga meli kubwa katika Ziwa Victoria bila kuomba mkopo popote,” amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli ameongeza kuwa wabunge wa Afrika Mashariki wanaowajibu wa kuhakikisha wanalinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya Jumuiya hiyo.
Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana na Jumuiya hiyo Rais Magufuli amesema kuwa kabla ya kuanza kwa umoja wa forodha mwaka 2005 biashara kati ya nchi wanachama ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.8 lakini baada ya kuanzishwa kwa umoja wa forodha imeongezeka hadi kufikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5.
Mbali na hayo Rais,  Magufuli ameshukuru uamuzi wa bunge hilo kufanyika mjini Dodoma ambapo kwa sasa Serikali imehamishia shughuli zake zote katika mkoa huo, na tayari watumishi wa serikali zaidi ya 3000 wameshahamia huku Rais Magufuli akitarajiwa kuhamia muda wowote mwaka huu.


Kwa upande wake Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Martin Ngoga amesema Bunge hilo linasubiri marekebisho ya mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ili  lugha ya Kiswahili ianze kutumika kama lugha rasmi katika vikao vya bunge hilo na katika jumuiya hiyo kwa kuzingatia azimio lililokwishapitishwa.
“Hatuoni sababu ya kutumia lugha za wageni wakati kuna lugha yetu ambayo tunazungumza ambayo ni kiswahili,” alisema Dkt. Ngoga.
Bunge la Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake mkoani Dodoma katika ukumbi mdogo wa Bunge wa Pius Msekwa. Bunge hilo limefanyika kwa mara ya kwanza mkoani humo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Martin Ngoga (kulia) pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai , (kushoto), mara baada ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki, (EALA) mjini Dodoma Aprili 24, 2018.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma. Kulia ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingia katika ukumbi wa Msekwa kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki mjini Dodoma.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiungana na  wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA) kuimba wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa katika ukumbi wa Msekwa, Bungeni mjini Dodoma.


  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki (EALA).


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika mkoni Dodoma.






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa tatu kutoka kulia, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Martin Ngoga wa nne kutoka kulia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuwahutubia mjini Dodoma. (PICHA NA IKULU)



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT MAGUFULI, EAC TUNAWEZA KUJITEGEMEA.
RAIS DKT MAGUFULI, EAC TUNAWEZA KUJITEGEMEA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCS-t4jQLXsGkYOrdRG9GL9w4nwfC2-rn8kGRvf_qJCrcTKzcM3unBJd-Gc7QHnQUIqgEkTKVhSIcwhN0hEzcGU9zCiKtWEBZIC1v-ugL-js_AHuKdCfzJekqDwKBqMEEzQQ6CrZWQhl0/s640/12.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCS-t4jQLXsGkYOrdRG9GL9w4nwfC2-rn8kGRvf_qJCrcTKzcM3unBJd-Gc7QHnQUIqgEkTKVhSIcwhN0hEzcGU9zCiKtWEBZIC1v-ugL-js_AHuKdCfzJekqDwKBqMEEzQQ6CrZWQhl0/s72-c/12.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/rais-dkt-magufuli-eac-tunaweza.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/rais-dkt-magufuli-eac-tunaweza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy