Wananchi wakisikiliza elimu ya kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati kutoka timu ya Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Halmashauri na Ofisi y...
 |
Wananchi wakisikiliza elimu ya kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa
wakati kutoka timu ya Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Halmashauri na Ofisi ya Kanda
ya Ardhi ya Kaskazini katika eneo la Kilombero, Jijini Arusha
|
 |
| Ofisa Mwandamizi wa Ardhi kutoka Kanda ya Kaskazini; Bwn. Thadeus Riziki akitoa Elimu ya ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati katika eneo la Sakina kwa Iddi, Jijini Arusha |
 |
Bwn. Juma Muhando, mwananchi wa eneo la Osunyai, akiuliza swali kwa Ofisa Ardhi Mwandamizi wakati wa utoaji elimu ya ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi katika eneo la Kilombero, Jijini Arusha
|
 |
| Wananchi wakipokea Vipeperushi vinavyoonyesha ulipaji wa Kodi ya pango la Ardhi Kielektroniki kwa mfumo wa GEPG katika eneo la Mbezi Dampo, jijini Arusha |
 |
| Wasanii wa kuhamasisha ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi, wakiwa katika tukio la kuhamasisha kufanya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati kwa njia ya Kielektroniki katika eneo la Morombo, Jijini Arusha. |
 |
| Zoezi la kubandika Stika za elimu ya kulipa Kodi ya Pango la Ardhi Kielektroniki kwa mfumo wa GEPG katika Dala dala na Maeneo ya Sokoni lilivyokuwa likiendelea Jijini Arusha. |
 |
| Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kaskazini, Bwn. Leo Komba akiwa Kili Radio – Moshi akitoa Taarifa kwa Wananchi wa Kanda ya Kaskazini kuhusu kuzingatia wakati wa Neema (Grace Period) uliotolewa na Mhe. Waziri wa Ardhi; William Lukuvi wa kumtaka kila mmiliki wa Ardhi kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kabla ya tarehe 30 Aprili ili kuepuka kupelekwa Mahakamani. |
 |
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kaskazini, Bwn. Leo Komba akitoa Taarifa kwa Vyombo vya habari kuhusu kuzingatia wakati wa Neema (Grace Period) uliotolewa na Mhe. Waziri wa Ardhi; William Lukuvi la kumtaka kila mmiliki wa Ardhi kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kabla ya tarehe 30 April ili kuepuka kupelekwa Mahakamani. (Na Mboza Lwandiko – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi)
|
|
COMMENTS