MTOTO WA MKULIMA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA ATAJA MUAROBAINI WA KUZUIA UCHOMAJI MISITU
HomeJamii

MTOTO WA MKULIMA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA ATAJA MUAROBAINI WA KUZUIA UCHOMAJI MISITU

  Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, "Mtoto wa Mkulima" akionyesha furaha yake baada ya kuzindua nembo ya "Malkia wa...

POLISI TAZARA WATOA ONYO KWA WAHALIFU.
RAIS DKT. MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE YA SH. MILIONI 60 KWA WAJUMBE WA CHAMA CHA WALIMU PAMOJA NA WANAFUNZI WA UDOM WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO CWT
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, ABDALLAH ULEGA AZ AKIZINDUA ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO



 Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, "Mtoto wa Mkulima" akionyesha furaha yake baada ya kuzindua nembo ya "Malkia wa Ssali" kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma leo Aprili 14, 2018.




NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA


WAKATI
kuna wimbi la uchomaji misitu ovyo hapa nchini, “Mtoto wa Mkulima, Waziri Mkuu
Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda ametoa “dawa” ya kuzuia uharibifu huo wa maliasili
na si nyingine bali ni kufuga nyuki.
Waziri
Mkuu huyo mstaafu ambaye alipenda kujitambulisha kama mtoto wa mkulima kutokana
na mapenzi yake katika Kilimo, alitoa “elimu” hiyo leo Aprili 14, 2018 wakati
akizindua nembo ya “Malkia wa Asali Tanzania” kwenye Hoteli ya Morena mjini
Dodoma.
“Sisi
upande wa Katavi tulichofanya, nilmwambia mkuu wa Mkoa sisi kuchoma choama misitu
ni “tradition” (utamaduni) yaani
kuchoma ni jambo la kawaida na ukitaka kuzuia hili jaribu kutumia ufugaji wa
nyuki kama silaha ya kuzuia uchomaji wa miti.” Alisema na kuendelea.
Kwa
hivyo alichofanya maeneo kama Inyonga, tulitenga maeneo na kuweka mabango yetu tukaweka
wafugaji wa nyuki na kuwaambia ninyi ndio walinzi wetu na tangu tufanye hivyo
kumekuwepo na hali nzuri sana, na uchomaji moto umepungua sana, alisema.
Mheshimiwa
Pinda alitoa mfano mwingine jijini Mbeya (Mbeya city), ambako mji umezungukwa
na milima mizuri yenye misitu ambayo imekuwa ikiharibiwa na uchomaji moto mara
kwa mara.
“Alitokea
baba mmoja Askofu Mwalyego siku moja akaja kuniambia baba mimi hii inanikera
kama inavyokukera sana wewe, hivi nikijaribu ku-introduce ufugaji wa nyuki hapa
itasaidia, nikamwambia try (jaribu),
ameweka wafugaji wa nyuki  kuzunguka
milima pale Mbeya mjini na mimi nikamwambia I
will buy all your honey
na juzi nikawa namuuliza zoezi langu linakwendaje,
akaniambia nina miaka miwili mitatu sijaona moshi kwenye lile eneo.
Kutokana
na uzoefu huo  Mtoto wa Mkulima akatoa
hakikisho kuwa “Hii ni silaha moja nzuri kwa sababu mtu akielewa halimpi shida
hata kidogo.” Alisema.
Mhe.
Pinda pia alisema, ufugaji nyuki pia ni silaha ya kuzuia ujangili wa wanyama na
kutolea mfano wa hifadhi ya misitu huko Kigoma na alipokutana na CEO pale
masikitiko yake makubwa ilikuwa ni sula la ujangili na ushauri wangu
nilimwambia akae na wafugaji nyuki, walau kuzunguka eneo hiulo la misitu.
“Yule
bwana alijaribu na nilipomtembelea mara ya pili aliruhusu wafugaji na mfugaji
bwana ukimwambia ukimwambia ukiruhusu kuingia hapa mtu ambaye hatumjui
tunakufukuza hapa unaondoka na anajua ndoo moja laki moja inamkosa hakubali na
kwakweli wamefanya kazi nzuri na amewafanya sasa kama askari wa wanyamapori.”
Alifafanua
Akizungumzia
faida ya asali, Mhe. Pinda alisema ni chakula kilichobeba virutubisho vyote
ambavyo binadamu anahitaji lakini si hivyo tu, asali imekuwa na soko kubwa
ulimwenguni na inaweza kuwa chanzo kimoja cha kukuza uchumi kwa wananchi na
taifa kwa ujumla.
“Nawaomba
sana waheshimiwa wabunge, mimi nilishatoka huko, lakini bwana Camara hapa
anachohitaji ni visemeo juu ya umuhimu wa sekta hii, ni sekta ndogo lakini
mchango wake unaweza kusaidia sana katika uchumi.
Aidha
Mheshimiwa Pinda alisema, nchi yetu imejaliwa kuwa na eneo kubwa sana la misitu
kuliko nchi nyingi na kusikitishwa wakati alipokwenda Addis-Ababa Ethiopia ambapo
aliposoma jarida, aliona eti Ethiopia ndio namba moja kwa uzalishaji asali
barani Afrika, nikamwambia Camara hivi Ethiopia ina uoto gani wa asili wa
kuizidi Tanzania?
Alisema,
mahitaji ya asali Tanzania  ni zaidi ya
tani 140,000 na anaamini ni zaidi lakini Tanzania inatoa asali kidogo sana, na
Ethiopia wanazalisha tani 40,000 wakati yeye (Pinda) Tanzania inazalisha tani
24,000 tu.
Nembo
hiyo iliyozinduliwa ni ya kampuni ya Nyuki Safari ambayo iko chini ya Mtanzania
Kaizirege David Camara na Mmarekani Mary Winzer Canning na lengo lake ni
kuboresha bidhaa hiyo ya asli ili kuvutia soko.


Mhe. Pinda akiangalia Mvinyo (wine), uliotengenezwa na kampuni ya Nyuki safari ikiwa na nembo mpya ya Malkia wa Asali.
Mhe. Pinda akiungana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Kuandikwa, (wapili kulia), Mbunge wa Urambo, Mhe. Margareth Sitta, (wakwanza kushoto), Mwanzilishi mwenza na Afisa Mkuu Mbunifu wa kampuni ya kuzalisha asali ya Nyuki Safari, Mary Winzer Canning, (wanne kushoto), na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Profesa Silayo na mrembo aliyebeba nembo hiyo. 




 Mhe. Pinda na wageni wengine wakishiriki kwenye uzinduzi wa nembo hiyo.




 Mhe. Pinda wakati akitoa hotuba yake.
 Mhe. Pinda katika picha ya pamoja na Waanzilishi wenza wa kampuni ya Nyuki Safari, Bw.Kaizirege David Camara, (kushoto), na Bi. Mary Winzer David Canning.
 Bw. Kaizirege akizungumza.
 Mhe. Pinda, (katikati), Mama Sitta ba Bi. Mary




 Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino, Bw.Paschal Masatu, akitoa hotuba yake
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Profesa Silayo, akizungumza.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MTOTO WA MKULIMA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA ATAJA MUAROBAINI WA KUZUIA UCHOMAJI MISITU
MTOTO WA MKULIMA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA ATAJA MUAROBAINI WA KUZUIA UCHOMAJI MISITU
https://i.ytimg.com/vi/FgVSE27Fmt0/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/FgVSE27Fmt0/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mtoto-wa-mkulima-waziri-mkuu-mstaafu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mtoto-wa-mkulima-waziri-mkuu-mstaafu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy