HomeJamii

MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wajiepushe na tabia ya kuingiza siasa katika suala la kuwaondoa wananchi waishio mabond...

MAKAMU WA RAIS AWATAKA VIJANA WASOMI KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO DKT. TITO MWINUKA AWAHAKIKISHIA WATANZANIA MRADI WA UMEME WA GESI ASILIA WA KINYEREZI II UNAENDELEA KWA KASI
UNESCO YATOA TAHADHARI ONGEZEKO LA JANGWA



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wajiepushe na tabia ya kuingiza siasa katika suala la kuwaondoa wananchi waishio mabondeni  kwa kuwa jambo hilo linafanywa kwa maslahi ya wananchi wenyewe.



Amesema wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha na mali zao kila yanapotokea mafuriko, hivyo ni vizuri kwa viongozi wakiwemo wabunge washirikiane na Serikali kuwahamasisha wakazi wote wa mabondeni wahame.

Waziri Mkuu ameyasema hayo Alhamisi, Aprili  19, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Temeke, Bw. Abdallah Mtolea katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

 “Mara nyingi Serikali imekuwa ikiwataka wakazi ya maeneo ya mabondeni kuhama  ila suala hilo limekuwa likikwamishwa na masuala ya kisiasa. “Wabunge ni mashahidi jambo hili linapoamuliwa, zinaingizwa siasa.”

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wananchi walioathiriwa na maafa yaliyosababishwa na mafuriko zikiwemo familia za watu 12 waliofariki mkoani Dar es Salaam.

Katika swali lake, Bw Mtolea alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kudhibiti madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dar es Salaam.

Mapema akijibu swali la Mbunge wa Nyang’hwale , Bw. Hussein Nassoro Waziri Mkuu alisema suala la kurejesha miundombinu iliyoharibika linashughulikiwa na kamati za maafa za mikoa na wilaya ambazo kwa sasa zinafanya tathmini ili kujua kiwango cha uharibifu na hatua gani zichukuliwe.

Bw. Nassoro alitaka kujua Serikali imejipangaje katika kurejesha miundombinu iliyoharibika kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa wito wa wananchi kuhakikisha wanatumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbalimbali ya biashara na chakula. Kuhusu mazao ya biashara amesema Serikali itawasaidia kutafuta masoko.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Bi. Aida Khenani (Viti Maalumu), aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kuandaa masoko ya uhakika kwa mazao ya wakulima.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, APRILI 19, 2018.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA
MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/msiingize-siasa-suala-la-mabondeni.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/msiingize-siasa-suala-la-mabondeni.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy