MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI MSAADA WA VITANDA KWA KITUO CHA AFYA
HomeMikoani

MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI MSAADA WA VITANDA KWA KITUO CHA AFYA

  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akiongea na baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria katika hafla ya kukabidhi vifaa ...




 Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akiongea na baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria katika hafla ya kukabidhi vifaa na gari la kubebea wagonjwa kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya katika jimbo hilo 

 Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akikabidhi vitanda kwa ajili ya kituo hicho

Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akikabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa ajili ya kituo hicho 





NA FREDY MGUNDA, MUFINDI

MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ametoa msaada wa vitanda kumi kwa kituo cha afya cha Ihongole kilichokuwa kinakabiliwa na upungufu wa vitanda katika wodi ya wazazi. 

Akizungumza wakati kukabidhi vitanda hivyo sambamba na kukabidhi gari dogo la kubebea wagonjwa iliyotolewa na serikali, Chumi alisema kuwa msaada huo wa vitanda utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto
katika kituo hicho cha afya ambacho kinachohudumia wakazi zaidi ya 20000 wa
jimbo la Mafinga mjini. 

Alisema kuwa ushirikiano katika kuondoa changamoto na
kuchukulia mapungufu ndio njia pekee ya kuendelea kuinyanyua Mafinga hasa
katika sekta ya afya ambayo imekuwa ikikabiliana na changomoto nyingi.

Chumi alisema kuwa msaada wa vitanda vimetolewa na mmoja
wa wahisani wanaolisaidia jimbo la Mafinga kuondokana na changamoto mbalimbali
katika sekta ya afya ambayo imekuwa na ikikabiliwa na mapungufu mbalimbali
ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu bora.
  
Alisema changamoto za sekta ya afya katika jimbo hilo na
wilaya ya Mufindi kwa ujumla zitakashughulikiwa kupitia serikali na wadau wake
mbalimbali wanaotakiwa kujitokeza kuboresha huduma zake 

Akizungumzia Gari hiyo ambayo imetolewa na Serikali Chumi
alisema kuwa itatumika kubeba wagonjwa ambao watalazimika kukimbizwa kwenye
Hospitali ya Mafinga ambapo awali ilikuwa vigumu kwa wagonjwa pindi wakizidiwa kwenda kutibiwa. 

Mbali na msaada huo, mbunge huyo ambaye mbali na ahadi mbalimbali kwa wapiga kura wake, aliahidi kuboresha huduma za afya katika jimbo
hilo amekwishatoa msaada vitanda, magodoro, viti vya kubeba wagonjwa na vifaa
tiba mbalimbali katika hospitali ya Mafinga. 

Akipokea na kushukuru kwa msaada huo, Kaimu Mganga Mkuu wa kituo cha Ihongole, Bernad Makupa alisema msaada huo wa vitanda na gari ya kubebea wagonjwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwahudumia wananchi katika vijiji mbalimbali vinavyopata huduma katika kituo hicho.


Kwa niaba ya halmashauri ya Mafinga Mjini, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Charles Makoga alimshukuru Chumi kwa ushiriki wake katika kuchangia maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo kabla na baada ya kuingia
madarakani na akamuomba endelee na moyo huo.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI MSAADA WA VITANDA KWA KITUO CHA AFYA
MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI MSAADA WA VITANDA KWA KITUO CHA AFYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhWCrIj4W3Izjl1bo80oh3__4Qz8FFQUZb9W_CGOInNnDAKA8Oxss2XPy6Z2hGAeD3F758GnpYih0xgNx3pa_38DMNLWrTeH4adnbxa62kctKg4NTeP9oWJnpHRXVDEaVbzVCSP-yvPbc3O/s640/IMG-20180415-WA0416.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhWCrIj4W3Izjl1bo80oh3__4Qz8FFQUZb9W_CGOInNnDAKA8Oxss2XPy6Z2hGAeD3F758GnpYih0xgNx3pa_38DMNLWrTeH4adnbxa62kctKg4NTeP9oWJnpHRXVDEaVbzVCSP-yvPbc3O/s72-c/IMG-20180415-WA0416.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mbunge-cosato-chumi-akabidhi-msaada-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mbunge-cosato-chumi-akabidhi-msaada-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy