Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshikilia chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine) wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem, wengine pichani ni mabinti waliokuwa wa kwanza kupatiwa chanjo hiyo wakati wa uzinduzi, kushoto ni Neema Felix (14) mkazi wa Mbagala na mwingine ni Hadija Bakari (14) mkazi wa Kigamboni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewaagiza Waganga Wakuu na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kupima saratani ya matiti nay a mlango wa kizazi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi mkoani Dar es Salaam ambapo hafla ya uzinduzi zilifanyika kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala, wilaya ya Temeke.
Makamu wa Rais amesema Utoaji wa Chanjo dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi pamoja na uchunguzi wa awali kwa pamoja vitasaidia kuwakinga mabinti na kubaini mapema ugonjwa wa saratani kwa wanawake na hivyo kuepusha maumivu makali ama vifo vinavyoweza kuzailika
“ Tunatakiwa hadi Desemba, 2018 tuwe tumewafikia wanawake milioni tatu. Hii itawezekana endapo kila mmoja wetu ataweka kipaumbele katika kufikia lengo hilo.” Alisisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali itatoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi bila malipo yoyote katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo vya Serikali, Mashirika ya Dini na Taasisi Binafsi.
Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14 ni walengwa wa kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka huu 2018 ambapo jumla ya wasichana 6,16,734.
Makamu wa Rais ambaye aliwaeleza wananchi waliojitokeza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi kuwa anaunga mkono uwepo wa chanjo hiyo huku akitoa sababu mbili moja ikiwa ni kulinda jeshi la wanawake nchini Tanzania kwani wengi wamekuwa wakipoteza maisha yao kwa sababu ya Saratani na sababu ya pili ni kwamba Mama yake Mzazi alifariki kwa kansa hiyo ya saratani ya mlango wa kizazi.
Wakati huo huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania imeandika historia nyingine katika sekta ya afya kwa kuzindua chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa Kizazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshikilia chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine) wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem, wengine pichani ni mabinti waliokuwa wa kwanza kupatiwa chanjo hiyo wakati wa uzinduzi, kushoto ni Neema Felix (14) mkazi wa Mbagala na mwingine ni Hadija Bakari (14) mkazi wa Kigamboni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine) kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Aprili 10 2018. Kulia ni mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) na wageni maalum waliohudhuria wa tukio hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua chanjo ya saratani ya kizazi (HPV Vaccine), jijini Dar es Salaamleo. Pamoja naye (kulia kwake) ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na wageni maalum waliohudhuria wa tukio hilo.
24: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Binti mwenye umri wa miaka 14 anayefahamiaka kwa jina Hadija Bakari mkazi wa Kigamboni akichomwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine) wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mkazi wa Kigamboni na Neema Felix (14) mkazi wa Mbagala kijarida alipozindua chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine), jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na wahudhuriaji wa tukio hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi kipeperushi Hadija Bakari (14) mmoja wa mabinti wa kwanza kupata chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine), jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mabinti wa kwanza kupata chanjo ya ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine), aliyesimama (kushoto) ni Hadija Bakari (14) mkazi wa Kigamboni na Neema Felix (14) mkazi wa Mbagala.
Loaded All PostsNot found any postsVIEW ALLReadmoreReplyCancel replyDeleteByHomePAGESPOSTSView AllRECOMMENDED FOR YOULABELARCHIVESEARCHALL POSTSNot found any post match with your requestBack HomeSundayMondayTuesdayWednesdayThursdayFridaySaturdaySunMonTueWedThuFriSatJanuaryFebruaryMarchAprilMayJuneJulyAugustSeptemberOctoberNovemberDecemberJanFebMarAprMayJunJulAugSepOctNovDecjust now1 minute ago$$1$$ minutes ago1 hour ago$$1$$ hours agoYesterday$$1$$ days ago$$1$$ weeks agomore than 5 weeks agoFollowersFollowTHIS CONTENT IS PREMIUMPlease share to unlockCopy All CodeSelect All CodeAll codes were copied to your clipboardCan not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy
COMMENTS