JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFUNGA MAFUNZO YA UZAMIAJI MAJINI KINA KIREFU.

Mafunzo haya yalianza rasmi tarehe 19/04/2018 kwa jumla ya Askari 15, na yamewezeshwa na Wakufunzi kutoka taasisi ya SES iliyopo nchini Ujer...

Mafunzo haya yalianza rasmi tarehe 19/04/2018 kwa jumla ya Askari 15, na yamewezeshwa na Wakufunzi kutoka taasisi ya SES iliyopo nchini Ujerumani. Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Askari, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu hasa katika kukabiliana na majanga ya mafuriko na kuzama kwa watu majini haswa kwenye kina kirefu.



Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage, akipokelewa na Maafisa wa Jeshi hilo pamoja na mwenyeji wake ambaye ni mmiliki wa Yatch Club Bw. Brian Fernandes, alipokwenda kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika katika kisiwa cha Bongoyo kilichopo ndani ya bahari ya hindi, Jijini Dar es Salaam.


Mzamiaji wa kikosi maalum cha Uokoaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajini Gift Longwe, akionesha mbinu mbalimbali za uzamiaji majini kwenye kina kirefu walizojifunza toka kwa wakufunzi kutoka nchini Ujerumani,  kwa mgeni rasmi Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, (CF) Billy Mwakatage (hayupo pichani). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam.


Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (katikati), akimkabidhi cheti mmoja ya wahitimu wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu, Sajini Gift Longwe (kushoto). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam.


Wazamiaji wa kikosi maalum cha Uokoaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajini Gift Longwe (kushoto) na Koplo Siwizan Kazimoto (kulia), wakionesha umahili wao wa uzamiaji majini kwenye kina kirefu mbele ya mgeni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, (CF) Billy Mwakatage (hayupo pichani). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)







COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFUNGA MAFUNZO YA UZAMIAJI MAJINI KINA KIREFU.
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFUNGA MAFUNZO YA UZAMIAJI MAJINI KINA KIREFU.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyjvgDcfi-G0uizb3J2Lwlcps-mDZDQeSN_JH4o5tprap766rsHPdUvhp4KiBJPNL1XGILs4ckNg4dg8GBcM9l8ORXAnFeqQxatIlrnXcD5RrWZuXmH8s_WrlQ4Q_E0_rjKH3n_y2Kd7s/s640/PIX+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyjvgDcfi-G0uizb3J2Lwlcps-mDZDQeSN_JH4o5tprap766rsHPdUvhp4KiBJPNL1XGILs4ckNg4dg8GBcM9l8ORXAnFeqQxatIlrnXcD5RrWZuXmH8s_WrlQ4Q_E0_rjKH3n_y2Kd7s/s72-c/PIX+1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/jeshi-la-zimamoto-na-uokoaji-lafunga.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/jeshi-la-zimamoto-na-uokoaji-lafunga.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy