ECOBANK GROUP WASHIRIKIANA NA MTN KUWEZESHA HUDUMA ZAIDI ZA FEDHA BARANI AFRIKA

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya simu MTN imeingia ubia na moja ya benki inayoongoza barani Afrika ya Ecobank Transnational Incorporated (E...




Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya simu MTN imeingia ubia na moja ya benki inayoongoza barani Afrika ya Ecobank Transnational Incorporated (ETI) kuwezesha wateja wao kufaidika na huduma za kifedha zinazotolewa na makampuni hayo.

Imeelezwa kuwa MTN ikijivunia idadi kubwa ya wateja wanaotumia huduma zake mbalimbali; mtandao mkubwa wenye uhakika; bidhaa zenye ubunifu na huduma zake za kifedha kwa mtandao imeungana na Ecobank kuwezesha wateja wao kuanzisha kufungua akaunti na kupitisha miamala yao kupitia mtandao wa MTN.
Kutokea (kushoto) kwenda Kulia ni Charles Kie, Mkurugenzi Mtendaji wa, Ecobank Nigeria Ltd; Serigne Dioum, Mtendaji wa MTN’s , Hudma za kifedha kwa njia ya mtandao; Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa, Ecobank Transnational Incorporated (ETI), Rob Shuter, Ofisa Mtendaji mkuu wa MTN na Patrick Akinwuntan, Mtendaji wa Ecobank Transnational Incorporated (ETI)

Makampuni hayo mawili maarufu barani Afrika yametiliana saini mkataba wa makubaliano utakaowezesha kushirikiana katika kubuni na kuwezesha huduma za kifedha zenye ubora wa kiwango cha juu kati ya benki hiyo na mtandao wa simu wa MTN.

Miongoni mwa huduma zitakazotolewa ni kuwezesha miamala mbalimbali kufanyika kwa kutumia simu na akaunti za benki.

Kutumia mitaji iliyopo katika uwekezaji ndani ya Ecobank na MTN kuwezesha miamala ya kimataifa kufanyika kidigitali.

Aidha makubaliano hayo yatachochea ubunifu wa bidhaa mbalimbali katika upande wa hifadhi ya fedha kwa njia ya mtandao na ukopeshaji wake na kutoa nafasi ya malipo kwa njia ya mtandao kwa wateja, wafanyabiashara na mashirika mbalimbali.

Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank anasema: “ Mabadiliko ya kidigitali katika mifumo ya benki na simu kunatengeneza fursa za namna bora ya kuwezesha kutoa huduma za kifedha. Afrika inalazimika kwenda mbio katika digiti ili kuwezesha fursa zilizopo zitumike kuwatumikia wateja. MTN na Ecobank leo wamechukua hatua kubwa kuwezesha fursa hizo” .

Pia alisema kwamba mkakati wa benk hiyo wa kidigiti kwa muda mrefuj umelenga kuhakikisha nafuu ya uwezeshaji wa miamala katika soko.

Akizungumzia ushirikiano huo Ofisa Mtendaji Mkuu na Rais, Rob Shuter alisema: “Ushirikiano kati ya mabenki na watoaji wa huduma za miamala kwa njia ya simu ni muhimu, hivyo uhusiano wetu wa muda mrefu na Ecobank umelenga kuwezesha huduma za fedha kuwafikia wananchi wengi na kwa urahisi zaidi. Tumefurahishwa na maafikiano haya kwani yametupeleka hatua nyingine, kwani ushirikiano wetu utawezesha ubunifu utakaowezesha huduma za fedha kupenya kila mahali katika bara hili.”

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: ECOBANK GROUP WASHIRIKIANA NA MTN KUWEZESHA HUDUMA ZAIDI ZA FEDHA BARANI AFRIKA
ECOBANK GROUP WASHIRIKIANA NA MTN KUWEZESHA HUDUMA ZAIDI ZA FEDHA BARANI AFRIKA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigtlqa7gfsMNykg_f9ONgaSV_eTUegokSw-L9AV59EYLAKqHQeW8GZfOz0WwfzVIcG3OGyfgsFPHvztEJbPuXm_RfEfydiqzFTnL7ZQ-kMKAEjGLQ3jMwi75oElkyjWDN2b0hfnTCcyYw/s640/ecobank+na+MTN.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigtlqa7gfsMNykg_f9ONgaSV_eTUegokSw-L9AV59EYLAKqHQeW8GZfOz0WwfzVIcG3OGyfgsFPHvztEJbPuXm_RfEfydiqzFTnL7ZQ-kMKAEjGLQ3jMwi75oElkyjWDN2b0hfnTCcyYw/s72-c/ecobank+na+MTN.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/ecobank-group-washirikiana-na-mtn.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/ecobank-group-washirikiana-na-mtn.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy