HomeJamii

WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA

*Asisitiza kwamba kazi ndiyo msingi wa maendeleo  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na ma...

KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA TIGO YAKABIDDHI MSAADA KITUO CHA YATIMA MKOANI DODOMA
WAZIRI MWAKYEMBE AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI NAHODHA WA SERENGETI BOYS
DG WA PPF WILLIAM ERIO AUNGANA NA WAFANYAKAZI KUHUDUMIA WAWANACHAMA WA MFUKO, KATIKA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA








*Asisitiza kwamba kazi ndiyo msingi wa maendeleo 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Pia amewasihi wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani wahakikishe suala la kulinda mipaka hiyo linapewa kipaumbele ili kuimarisha amani na utulivu nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wananchi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.

Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ili vijana waweze kupata maendeleo lazima wafanye kazi kwa bidii.

Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani washirikiane na Serikali katika kuimarisha ulinzi na usalama. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ukarabati wa kituo cha afya cha Kata ya Mbekenyera na kuwaeleza wananchi dhamira ya Serikali ya kuwahudumia.

Amesema Serikali imetoa sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya kujifungulia, maabara, wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha upasuaji.
 “Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.
Pia, Waziri Mkuu amekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika kituo hicho. Gari hilo limetolewa na Rais Dkt. John Magufuli ili kuimarisha huduma za afya kituoni hapo



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, MACHI 24, 2018.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA
WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA
https://i.ytimg.com/vi/YdlsjfboTJ0/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/YdlsjfboTJ0/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-mkuu-awataka-vijana-wafanye-kazi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-mkuu-awataka-vijana-wafanye-kazi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy