WAZIRI DKT HARRSON MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI JIJINI ARUSHA

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Cham...


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) unaofanyika kwa siku tano jijini Arusha.

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama
cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo ,Susan Mlawi akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas akizungumza katika mkutano hu unaofanyika katika Ukumbi wa mikuano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) ,Pascal Shelutete akitoa taarifa ya TAGCO kwa washiriki wa Mkutano huo .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akifuatilia hotuba zilizotolewa wakati wa mkutano huo.
Katika Mkutano huo pia kumetolewa Vyeti kwa Wadau walioshiriki katika kufanikisha mkutano huo .
Mmoja wa Wadau  waliosaidia katika kufanikisha mkutano huo akipokea cheti kutoka kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe. 
Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi,Dkt Harrison Mwakyembe ,Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

WAZIRI wa Habari,Utamaduni ,Sanaa
na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amewaagiza Maafisa Habari wote nchini kutekeleza
majukumu yao kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za serikali huku akiwataka
kuzingatia malengo ya kitaifa waliyojiwekea katika kikao kilichopita.

Mbali na agizo
hilo Dkt Mwakyembe pia amesema serikali haita wavumilia maafisa habari ambao hawatambui wajibu wao  huku akiwafananisha na maafisa habari hewa
 ambao wanageuza tovuti za Serikali kuwa magofu badala ya kuwa na habari
mbalimbali zenye tija na maendeleo kwa taifa la Tanzania.

Dkt Mwakyembe ameyasema hay oleo wakati akifungua kikao
kazi cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikali ,kinachofanyika katika
Ukumbi wa mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha kinachowakutanisha zaidi
ya Maafisa Habari zaidi ya 300 kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji
wa majukumu yao.

Katika kikao hicho kinachoenda
sambamba na Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini
(TAGCO)kinafanyika wakati kukiwa bado kuna changamoto katika kada ya maafisa
Habari wa taasisi za Umma ikiwemo uharaka wa ufikishaji wa taarifa za serikali
kwa umma .

Katika mkutano huo Mkurugenzi
Mkuu wa Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas amewakumbusha
washiriki wa mkutano huo kuenenda kimkakati huku akitoa nukuu za mcheza filamu
Mashuhuri nchini Marekani ,Anord Schwazniger .
Naye Mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa ,Tanzania ,Alvaro Rodriguez amesema serikali ina umuhimu mkubwa wa
kufundisha na kuhabarisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia zinazo
iunganisha Dunia .

“Umoja wa Mataifa unaiona
Tanzania ya leo na kesho yenye mafanikio mengi sana,Demkorasia ,kufikia uchumi
wa kati ,Elimu Bure,kupiga vita rushwa ni kati ya vitu vinavyoipa Tanzania sifa
ya nchi iliyo tayari kuleta maendeleo ya nchi kwa ajili ya wananchi.”alisema
Rodriguez.

Katika mkutano huo TAGCO ambacho
ni chama kisicho cha kiserikali (NGO) kikiwa na madhumuni ya kukuza Mawasiliano
na kuongeza Usambazaji wa  Taarifa ndani
ya serikali na kati ya serikali na Wananchi  kimekabidh vyeti kwa Wadhamini wa mkutano huo
ikiwemo Kampuni ya Clouds Media Group.














COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI DKT HARRSON MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI JIJINI ARUSHA
WAZIRI DKT HARRSON MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI JIJINI ARUSHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7_6lEwPLUAln2Qhh7Rosq9-1NKFlc-wJBQ2m2qk11UOUxXYaDAsFFo8IDVeTcgyYCoIrMTbQfklcQk6p3FovqvFcCPsgnbeh5a_8jhLV9izIwvoJJM55rfO6Kdw8VCi7YKVbfVfgRq76c/s640/E86A9735.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7_6lEwPLUAln2Qhh7Rosq9-1NKFlc-wJBQ2m2qk11UOUxXYaDAsFFo8IDVeTcgyYCoIrMTbQfklcQk6p3FovqvFcCPsgnbeh5a_8jhLV9izIwvoJJM55rfO6Kdw8VCi7YKVbfVfgRq76c/s72-c/E86A9735.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-dkt-harrson-mwakyembe-afungua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waziri-dkt-harrson-mwakyembe-afungua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy