WATENDAJI WA SERIKALI, TENMET, APHRC WAJADILIANA KUBORESHA ELIMU
HomeJamii

WATENDAJI WA SERIKALI, TENMET, APHRC WAJADILIANA KUBORESHA ELIMU

Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Edicome Shirima akizungumza kufungua mkutano wa wadau wa elimu ikiwa ni utek...

WAZIRI JAFO:SITAKI UKANJANJA KATIKA UJENZI WA STENDI YA MABASI MBEZI LUIS
TANZANIA YATAJWA KUWA BUSTANI YA EDEN NA CHIMBUKO LA MWANADAMU WA KALE DUNIANI
RAIS DKT. MAGUFULI AONGEA NA WANANCHI MIKUMI, AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA KIDATU –IFAKARA YENYE KM 66.9 NA DARAJA LA MTO RUAHA ENEO LA NYANDEO KIDATU
Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Edicome Shirima akizungumza kufungua mkutano wa wadau wa elimu ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Tixon Tuyangine Nzunda akizungumza katika mkutano wa wadau washiriki kwenye mradi wa kuboresha elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.
Mtafiti Mwandamizi na Kiongozi wa Kitengo cha Elimu na Uwezeshaji Vijana wa African Population and Health Research Center (APHRC) Moses Ngware akizungumza katika mkutano kwa wadau wa elimu ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Meneja Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bw. Nicodemus Shauri Eatlawe (kushoto) akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akichangia mada katika mkutano wa wadau washiriki kwenye mradi wa kuboresha elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.

Mmoja wa washiriki katika mkutano wa wadau washiriki kwenye mradi huo akichangia mada.

Mkutano huo ukiendelea.

Mkutano huo ukiendelea.


BAADHI ya watendaji wa Serikali, Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) na taasisi ya African Population and Health Research Center (APHRC) wamekutana na kufanya majadiliano ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao na wadau hao waliokutana leo mjini Dodoma, Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Edicome Shirima alisema Serikali imeliona tatizo la msongamano wa watoto mtaani na ndio sababu ya kuja na utaratibu wa elimu bila ada.

Alisema utaratibu wa elimu bila malipo haumnyimi mzazi kuendelea kumwezesha mtoto wake kupata chakula awapo shuleni, hivyo kama wazazi watakubaliana kuwawezesha wanafunzi wao kupata chakula kwa utaratibu mzuri wanaweza kufanya hivyo bila vikwazo kutoka serikalini.

"...Haijazuiliwa mzazi kumlisha mtoto wake shuleni, wazazi kuweka utaratibu mzuri wa kuwalisha watoto wao wanapokuwa shuleni kwa makubaliano haijazuiliwa...tusaidiane kuelimisha umma kwa hili," alisema Dk. Edicome Shirima.

Alisema mbali na Serikali kuondoa ada shuleni bado kuna wazazi hawapeleki watoto shule, hivyo kuwaomba wabunge kuanza mchakato wa kuja na sheria itakayowabana wazazi wa aina hiyo.

Kwa upande wake Meneja Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bw. Nicodemus Shauri Eatlawe akiwasilisha mada kwa wajumbe hao aliwataka kushirikishana mawazo ili baadaye kutoka na mapendekezo yatakayoboresha zaidi utekelezaji wa mradi huo wa kuboresha elimu kwa makazi yenye msongamano.

Alisema utafiti wa awali walioufanya kwa baadhi ya shule za maeneo ya mradi unaonesha kumekuwa na changamoto nyingi kwa wanafunzi kutokana na msongamano uliopo mashuleni jambo ambalo linahatarisha usalama kiafya kwa wanafunzi na hata kitaaluma katika masomo yao.

changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto na elimu inayotolewa katika maeneo ya miji yenye msongamano kwa kuanzia na Jiji la Dar es Salaam, mradi huo pia unaweza kuendelezwa katika miji ya mikoa mingine hapo baadaye.

Mradi huo utakao saidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam utakao tekelezwa kwa miaka miwili na unaweza kusabazwa katika maeneo mengine ya Tanzania yenye changamoto hizo.



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATENDAJI WA SERIKALI, TENMET, APHRC WAJADILIANA KUBORESHA ELIMU
WATENDAJI WA SERIKALI, TENMET, APHRC WAJADILIANA KUBORESHA ELIMU
http://s3-us-west-2.amazonaws.com/thehabari.com/wp-content/uploads/2018/03/17170512/IMG_3991-500x282.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/watendaji-wa-serikali-tenmet-aphrc.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/watendaji-wa-serikali-tenmet-aphrc.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy