RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA MAJAJI 10, WAKILI MKUU, MANAIBU MWANASHERIA MKUU, MKURUGENZI WA MASHITAKA NA WAKILI MKUU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz To...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 20 Aprili, 2018 amewaapisha Majaji 10 wa Mahakama Kuu, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka aliowateua tarehe 15 Aprili, 2018.
Majaji walioapishwa ni Mhe. Elvin Claud Mgeta, Mhe. Elinaza Benjamin Luvanda, Mhe. Yose Joseph Mlyambina, Mhe. Immaculata Kajetan Banzi, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani, Mhe. Paul Joel Ngwembe, Mhe. Agnes Zephania Mgeyekwa, Mhe. Stephen Murimi Magoiga, Mhe. Thadeo Marco Mwenempazi na Mhe. Butamo Kasuka Philip.
Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Dkt. Evaristo Emmanuel Longopa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Edson Athanas Makallo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Dkt. Julius Clement Mashamba kuwa Wakili Mkuu wa Serikali na Dkt. Ally Saleh Possi kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
Baada ya kuapishwa kwao, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kufanya uteuzi wa Majaji hao na kwamba uteuzi huo utasaidia kupunguza mrundikano wa mashauri ya Mahakama Kuu ambapo sasa Jaji mmoja atakuwa akisikiliza wastani wa mashauri 460 kwa mwaka ikilinganishwa na Jaji mmoja kusikiliza mashauri 535 kabla ya uteuzi huo.
Mhe. Prof. Juma amewahusia Majaji wapya umuhimu wa kuzingatia majukumu yao, miiko na kuwa mfano bora wa kusimamia sheria na pia ametoa wito kwa wananchi kuwa makini wanapopata taarifa za mahakama kutoka vyanzo visivyo rasmi kwani kumekuwa na upotoshaji wa makusudi.
“Mhe. Rais Bajeti yetu ya mwaka 2017/18 ilikuwa Shilingi Bilioni 125, bajeti tuliyopangiwa sasa 2018/19 ni Shilingi Bilioni 141, sasa wanaosema bajeti imeshuka, imeshuka kwa namna gani? labda ni kushuka kwa kugeuza. Kwa upande wa bajeti ya maendeleo kwa mwaka 2017/18 ilikuwa Shilingi Bilioni 18, mwaka huu tumepangiwa Shilingi Bilioni 35” amesisitiza Mhe. Prof. Juma.
Akizungumza baada ya salamu za Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Majaji na viongozi wote walioapishwa na ametoa wito kwao kutekeleza majukumu yao kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu, kuweka mbele maslahi ya Taifa na kutenda haki hasa kwa Watanzania wanyonge wakiwemo wajane na watu masikini ambao hudhulumiwa katika vyombo vya kutolea haki.
Mhe. Rais Magufuli ameungana na Jaji Mkuu wa Tanzania kuwatahadharisha Watanzania dhidi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kufanya upotoshaji wa taarifa na kuleta madhara katika jamii na ametaka Majaji na mamlaka nyingine zichukue hatua za kisheria dhidi ya wanaofanya upotoshaji huo.
Mhe. Rais Magufuli ametaja upotoshaji mmojawapo kuwa ni madai kwamba Serikali imeiba Shilingi Trilioni 1.5, na akamuuliza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Juma Assad ambaye amejibu sio kweli kwamba fedha hizo zimeibwa.
“Nilikuwa nasoma mahali wanasema Serikali imeiba Shilingi Trilioni 1.5, siku moja nikampigia CAG, kwamba mbona kwenye ripoti yako uliyonisomea Ikulu hukunieleza huu wizi wa Trilioni 1.5? Kwa sababu ungenisomea siku hiyo hiyo ningefukuza watu, kama nimefukuza wakurugenzi watatu siku hiyo hiyo kwa sababu ya hati chafu, hawa wa Trilioni 1.5 uliwaficha wapi? Nimejaribu kupita kwenye ripoti siioni mahali palipoandikwa zimepotea Trilioni 1.5, Prof. Assad akaniambia hakuna kitu kama hicho, nikamuuliza Katibu Mkuu akasema hakuna kitu kama hicho” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Viongozi wote walioapishwa pia wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela, na hafla ya kuapishwa kwao imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Makatibu Wakuu, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa dini.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

20 Aprili, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Thadeo Marco Mwenempazi mmoja wa wateule 10 walioapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Dkt. Ally Salehe Possi kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapongeza baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapongeza baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapongeza baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapongeza baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Ally Saleh Possi baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Jaji Kiongozi Mhe Ferdinand Wambali baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na waandishi wa habari wa ITV, Idrissa magomeni (kushoto) na Godfrey Monyo baada ya kuwaapisha Majaji Kumi wa Mahakama Kuu, Wakili Mkuu wa Serikali na Manaibu Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mshataka na Wakili Mkuu  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2018. (Picha na IKULU)


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA MAJAJI 10, WAKILI MKUU, MANAIBU MWANASHERIA MKUU, MKURUGENZI WA MASHITAKA NA WAKILI MKUU
RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA MAJAJI 10, WAKILI MKUU, MANAIBU MWANASHERIA MKUU, MKURUGENZI WA MASHITAKA NA WAKILI MKUU
https://lh3.googleusercontent.com/v7QvUf0J3oefXiaX7vJ7NJY4owPdvpzDppM0kLIS4xkJIvB2LkFlijyA4aRdzbxEe79Wy96KpYLdlnnwbnAvHuzRYzoFanFOTsik9Vvw9oqGM_rl6FT48EMbFeAgEGoSgyy9VajIe5igylxyFQ
https://lh3.googleusercontent.com/v7QvUf0J3oefXiaX7vJ7NJY4owPdvpzDppM0kLIS4xkJIvB2LkFlijyA4aRdzbxEe79Wy96KpYLdlnnwbnAvHuzRYzoFanFOTsik9Vvw9oqGM_rl6FT48EMbFeAgEGoSgyy9VajIe5igylxyFQ=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/rais-dkt-magufuli-aapisha-majaji-10.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/rais-dkt-magufuli-aapisha-majaji-10.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy