Mteja wa muda mrefu wa bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Manfred Ngantunga (kulia) akifu...
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Kulia ni Meneja Mkuu wa Woolworths Joehans Mgimba akiongea na wana habari wakati wa hafla ya uzinduzi huo. |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo |
**********
Na Mwandishi
Wetu
Katika kipindi msimu huu wa sikukuu ya Pasaka Watanzania wanaweza kununua nguo zenye ubora kwa nusu bei kufuatia punguzo la asilimi 50 lililotangazwa jana na duka maarufu la nguo la Woolworths jijnini Dar Es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
punguzo hilo, Meneja Mkuu Mkazi wa duka hilo Joehans Mgimba aliwaambia wateja
waliofika dukani hapo kuwa punguzo hilo litadumu kwa muda wa wiki nne.
Alisema lengo kubwa la Woolworths ni
kuwawezesha Watanzania wenye vipato vya aina mbali mbali kufurahia
sikukuu ya Pasaka kwa kupata nguo za kisasa zenye ubora kwa gharama nafuu.
Meneja huyo pia aliwaasa Watanzania kuachana na nguo za mtumba“Tunawasihi Watanzania kuepukana na
matumizi ya nguo za mtumba kwani si salama kwa afya zao. Katika kipindi hiki
cha sikukuu ya Pasaka duka la Woolworths linatoa punguzo kubwa ili kuwawezesha Watanzania kupata nguo mpya na zenye ubora.,” alisema.
Mgimba alisema duka hilo ambalo ni
moja kati ya maduka makubwa ya nguo hapa nchini, litaendelea kuwahudumia wateja
wake kwa kuwaletea nguo nzuri na zenye ubora kwa gharama nafuu na hivyo
kuwasaidia kuepukana na nguo za mtumba.
“Mteja anayekuja kununua nguo dukani
kwetu anakuwa amefanya uamuzi sahihi kwani atapa nguo zenye ubora kwa gharama
nafuu na atakuwa amepata kitu ambacho kinaendana na thamani ya pesa yake,”
alieleza
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, duka
hilo pia linatoa nafasi kwa wateja kununua nguo kwa kulipia kidogo kidogo hadi kwa
muda wa miezi mitatu ili kuwawezesha wale wasio na fedha za kutosha kulipa mara
moja kuweza kufurahia nguo zenye ubora.
Kuhakikisha wateja wetu wanapata vitu
bora kabisa, vinavyoendana na wakati na kwa mda muafaka, Woolworths imeweza
kubadilisha mfumo wa uletaji wa bidhaa nchini badala ya kutumia meli kama
zamani sasa inatumia usafiri wa ndege. Kabla ya hapo tulikuwa tunnatumia
muda wa mwezi mmoja hadi miwili kufikisha mizigo nchini wakati kwa sasa
tunatumia mda wa wiki mbili hadi tatu.
Bwana Mgimba pia akasisitiza kwamba
anapenda kuwahakikishia wateja wao kwamba Woolworths Tanzania ina bidhaa zote
kama zinazopatikana South Africa na kwa bei zinazofaa kabisa.
Kwa upande wake Manfred Ngatunga
ambaye ni mmoja kati ya wateja wazuri wa duka hilo alitoa shukrani zake kwa
uongozi wa duka hilo kwa kutoa punguzo kubwa haswa katika mismu huu wa sikukuu ya
Pasaka.
Uamuzi wa punguzo la bei umekuja
kipindi kizuri sana. Kipindi hiki na kipindi ambacho familia zinafanya manunuzi
kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka. Tunashukuru kwa kuwa tutapata nguo zenye ubora
kwa nusu bei, kila mtu sasa anaweza kupendeza,” alieleza.
COMMENTS