TIGO NA SAMSUNG WAUNGANA KUTOA SIMU YA SAMSUNG S9 NA SUMSUNG S9+ WATEJA WA TIGO

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waadishi wa habari katika hafla ya ushirikiano kati ya Tigo Tanzania na kam...



 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waadishi wa habari katika hafla ya ushirikiano kati ya Tigo Tanzania na kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwa ajili ya kuwapatia wateja wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo.  Wengine (kulia) Meneja wa Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed na Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Huduma wa Tigo, Davidi Umoh. Hafla ilifanyika Jijini Dar es salaam jana.


       Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Huduma wa kampuni ya Tigo, Davidi Umoh              katikati),  Meneja wa Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael wakizindua simu mpya za kisasa aina ya Samsung S9 na Samsung S9+ ambazo zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini kwa mara ya kwanza.


Simu ya Smartphone yenye GB 3 za internet bure kila mwezi kwa muda wa miezi sita kutoka Tigo.  

Tarehe 22 Machi 2018, Dar es Salaam.  

Wapenzi wa smatphone wanayo sababu nyingine ya kutabasamu baada ya kampuni inayoongoza ya mtindo wa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania kuungana na kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwaajili ya kuwapatia wateja wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo.  

'Tigo ni kampuni pekee ya simu za mkononi na ya kwanza kuwa na  simu mpya za kisasa za Samsung S9/S9+ nchini. Hakuna mwendeshaji mwingine yeyote wa mtandao wa simu au duka ambalo tayari limeshapokea simu hizi za kisasa za smartphone,' Mkuu wa idara ya Bidhaa na Hudumawa Tigo (Head of Products and Services), Davidi Umoh aliabainisha.  

Umoh aliongeza kuwa 'Tigo imeshika usukani wa mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidigitali . Tuna lenga katika kuendelea kuongeza upatikanaji wa simu za smartphone nchini wakati huo huo tukiwa tunahakikisha kuwa wateja wetu wote wanafurahia huduma bora za kidigitali kupitia mtandao wetu wenye kasi zaidi wa 4G ambao ndio uliosambaa zaidi hapa nchini.


Akielezea kuhusu Ushirikiano uliopo, Meneja wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Suleiman Mohammed  amesema"Tunajisikia fahari sana kushirikiana na Tigo kwaajili ya kuleta fursa za kusisimua na ofa kwa wateja wa Tanzania. Hii ni hatua ya msingi sana katika ukuzaji wa sekta ya simu za mkononi ambayo inaruhusu wateja kupata simu za kisasa katika wakati huo huo ambapo simu hizo zinazinduliwa duniani kote".  

Kuna njia tatu za kununua simu ya smartphone ya Samsung S9/S9+ Kwanza mteja anaweza kutembelea duka lolote la Tigo nchi nzima nakulipia na kujipatia simu mpya ya kisasa aina ya Samsung S9 na S9+. Njia ya pili ya kununua simu hizo nikutembelea Tigo Store katika ukurasa wa mtandao wa manunuzi wa jumia www.jumia.co.tz/tigo-shop. Mwisho wateja wanaweza kupiga menyu mpya ya Tigo *147*00# na kisha kuchagua duka la simu ambako utaweza kuchagua namna ya kulipia ambayo inaruhusu kulipia kidogo kidogo na kuchukua simu yake baadae.  

Simu za smartphone za kisasa za Samsung S9/S9+ zinapatikana katika rangi nyeusi, kijivu na zambarau na zitauzwa reja reja kwa bei ya TZS  2,049,000 kwa Samsung S9 na TZS 2,315,000 kwa Samsung S9+.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIGO NA SAMSUNG WAUNGANA KUTOA SIMU YA SAMSUNG S9 NA SUMSUNG S9+ WATEJA WA TIGO
TIGO NA SAMSUNG WAUNGANA KUTOA SIMU YA SAMSUNG S9 NA SUMSUNG S9+ WATEJA WA TIGO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLz2pHnPIePSGGsbV0qMylRVALIvdV518IgPw8tIo7YmyNBS2S1gl_Be7eTyRtVlJiL2kGZGoX-8Mc-P9fljIEuwnUJum-IW2UL_tig8Qr6BODVbFGyeJz6glb2S3D-oT3y4d_qWTUVWE/s640/10+%25282%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLz2pHnPIePSGGsbV0qMylRVALIvdV518IgPw8tIo7YmyNBS2S1gl_Be7eTyRtVlJiL2kGZGoX-8Mc-P9fljIEuwnUJum-IW2UL_tig8Qr6BODVbFGyeJz6glb2S3D-oT3y4d_qWTUVWE/s72-c/10+%25282%2529.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/tigo-na-samsung-waungana-kutoa-simu-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/tigo-na-samsung-waungana-kutoa-simu-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy