Kamatiya Bunge ya Miundombinu imeutaka Wakalawa BarabaraNchini (TANROADS), kujipanga nakuja na mikakati bora ya kuilinda miundombinu ya ...
Kamatiya Bunge ya Miundombinu imeutaka Wakalawa
BarabaraNchini (TANROADS), kujipanga nakuja na mikakati bora ya kuilinda miundombinu
ya barabara za lami inazozijenga hapa nchini ili ziwe fursa za kiuchumi badala ya
kuwa chanzo cha ajali.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Sulemani
Kakoso amesema hayo mara baada ya kamati
yake kutembelea ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Tabora KM 259 inayojengwa kwa
kiwango cha lami na kusisitiza kuwa umefika wakati kwa TANROADS kutoa elimu kwa
jamii za vijijini kuzilinda barabara zinazojengwa na kuzitumia fursa za uwepo barabara
za lami kujiletea maendeleo.
“Hakikisheni mnakuwa na programu endelevu za kuwaelimisha
wananchi umuhimu wa barabara za lami ili badala ya kuzihujumu kwa kuharibu miundombinu
ya barabara hizo wazilinde na kuzitumia kuibua fursa za kiuchumi na kijamii katika
maeneo yao”, amesema Mhe. Kakoso.
Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anaeshughulikia sekta ya Ujenzi Mhe. Elias John
Kwandikwa ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Serikali imejipanga kuufungua mkoawa Tabora
kwa kuhakikisha unafikika kwa pande zote kwa barabara za lami ili kuhuisha fursa
za uzalishaji na kukuza uchumiwa wananchi wake.
“Tumeigawa barabara hii katika sehemu tatu ili
kuharakisha ujenzi wake ambapo sehemu ya Manyoni- Itigi- Chaya KM 89.5 na Tabora–Nyahua
KM 85, ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika na sehemu ya Chaya-Nyahua
KM 85.4 mkandarasi anaendelea na ujenzi”, amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.
Nae meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Eng.
Leonard Kapongo na Tabora Eng. Damian Ndabalinzi wameihakikishia Kamati ya Bunge
ya Miundombinu kuwa watatekeleza utoaji elimu ya matumizi bora ya barabara na kudhibiti
maeneo yenye ajali nyingi katika mikoa yao ili jamii katika mikoa hiyo zinufaike
na uwepo wa barabara za lami.
Kamati ya Bunge ya Miundombinu iko katika ziara
ya kutembelea miundombinu inayosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma ili kujifunza na kushauri namna bora
ya kuendeleza miundombinu hapa nchini na hivyo kuwezesha malengo ya Tanzania
kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kutekelezeka.
(Imetolewa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini)
Muonekano wa barabara ya Nyahua –Tabora KM 85 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Manyoni-Itigi-Tabora KM 259 |
COMMENTS