TANESCO KUSAFIRISHA UMEME KUPITA ARDHINI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
HomeJamii

TANESCO KUSAFIRISHA UMEME KUPITA ARDHINI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

  Kaimu Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa u...

RAIS MAGUFULI AITAKA MAHAKAMA KUFUATILIA MADENI YA KESI SERIKALI ILIZOSHINDA
TRA YATOA WITO KWA WALIOCHELEWA KUHAKIKI TIN, YATAJA MIKOA INAYOFUATA KWA UHAKIKI
TAARIFA YA SERIKALI KUTOKA BUNGENI LEO 02/02/2017







 Kaimu Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines), kwenye shule ya sekondari ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2016.





NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO), limekamilisha
ujenzi wa  mfumo wa njia ya usafirishaji
umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) ,  kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya
Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda
kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV.
Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji
wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa
Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa  mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa
njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution Lines), wa
kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City
Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo, Railway na Sokoine.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi
alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi
(Underground Transmision Lines),  kwa
msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari umekamilika
na ule wa kutoka shule ya sekondari ya wasichana Jangwani kwenye City Centre
pia umekamilika.
“Faida kubwa ambayo wakazi wa jiji la
Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika (reliable power supply ulio
kwenye viwango stahiki, (Acceptable quality power supply) hususan kwa wale wa
maeneo ya katikati ya jiji,” Aliongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala,
Mhandisi Athanasius Nangali.
Akieleza zaidi, Mhandisi Nangai
alisema, “Mradi huu unaviwezesha viituo tajwa kuwa na njia mbili za kuvvipatia
umeme na hivyo kuwezesha kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia moja
kati ya hizo itakuwa na hitilafu.” Alifafanua.
Alisema kuongezeka kwa kituo cha City
Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo
9 vya aina hiyo.
“Hivi sasa tunaweza kusema, ujenzi
umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98, kinachoendelea ni kukamilisha ujenzi wa
mfumo wa njia ya kusafirisha umeme kupitia juu (Overhead Transmission Lines), wa
kilomita 1.3 wa msongo wa kilovolti 132 kutoka kituo kikubwa cha kupozea umeme
cha Ilala hadi shule ya sekondari ya wasichana Jangwani ambapo utaungana na
mfumo wa usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines)
kwenda kituo kikubwa cha City Centre.” Alifafanua.
kutoka Makumbusho kwenda kituo cha
City Centre, umekamilikakatikati yan jiji utekelezaji wa Mradi huo,
unaofadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Finland, unahusisha ujenzi
wa kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme (Distribution SCADA System),
katika msongo wa kilovolti 33 na 11.
“Tayari ujenzi wa kituo cha City
Centre umekamilika kwa asilimia 100 na sasa tuko katika hatua za majaribio.”
Alisema Mhandisi Rashidi.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa
TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba wakazi wa jiji kuwa wavumilivu wakati
zoezi hili la kuboresha miundombinu likiendelea kwani huwa panatokea kukatika
kwa umeme sehemu Fulani Fulani ili kutoa nafasi kwa mafundi kufanya kazi kwa
usalama zaidi.





 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala,  Mhandisi Athanasius Nangali, (katikati), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia), Afisa Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Hendry Kilasila, wakitembelea eneo la ujenzi wa Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam
 Hizi ndio njia za kusafirisha umeme ardhini zilizojengwa kwenye shule ya sekondari ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam
 Nguzo ya kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuja shule ya sekondari ya wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya jiji


 Mafundi wakiwa kazini




 Mhandisi  Nangali, (mbele), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Rashid, (kulia), wakiangalia moja ya roller lenye nyaya.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANESCO KUSAFIRISHA UMEME KUPITA ARDHINI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
TANESCO KUSAFIRISHA UMEME KUPITA ARDHINI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPkdBCffOO65yF-9pJdQJEG1Pk2pg_InCgz5oay5ci15lmSQPYu4HyENzQRYfcak5ZAzMIptiajeOT0pvp1ao8vsjXokYudtHihsmuYB6erzZ_Dj-8hDaK5mU1Ccqy45SDGKpbck78H1Y/s640/001.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPkdBCffOO65yF-9pJdQJEG1Pk2pg_InCgz5oay5ci15lmSQPYu4HyENzQRYfcak5ZAzMIptiajeOT0pvp1ao8vsjXokYudtHihsmuYB6erzZ_Dj-8hDaK5mU1Ccqy45SDGKpbck78H1Y/s72-c/001.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/tanesco-kusafirisha-umeme-kupita.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/tanesco-kusafirisha-umeme-kupita.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy