MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA MBEYA ATIWA MBARONI KWA MADAI AMESABABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akizungumza na watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya kufuatia tukio la mama mja...







Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akizungumza na watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya kufuatia tukio la mama mjamzito kifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mmoja wa watoa huduma hospitalini hapo hali iliyopelekea mtoto kupoteza maisha.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akimfariji Maria Solomoni ambaye alipoteza mtoto wake kwa uzembe wa muuguzi katika katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
 

Patricia Kisoti Muuguzi anayetuhumiwa kufanya uzembe uliosababisha Mama mjamzito kujifungua na mtoto wake kupoteza maisha katika hospitali ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Mkuu wa Wilaya Chunya Rehema Madusa akiwa na majonzi baada ya kumsikia mama aliyepoteza mtoto wake mara baada ya kujifungua kutokana na uzembe wa muuguzi katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
 

Baadhi ya watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya katika Mkutano na Mkuu wa Wilaya ya Chunya mara baada ya kutokea tukio la mama mjamzito aliyepoteza mtoto wakati akijifungua kutokana na uzembe wa mmoja wa wauguzi hospitalini hapo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani akizungumza kuhusiana na tukio hilo la kufanyiwa ukatili kwa mama mjamzito na mmoja wa wauguzi.


Wananchi na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya kikatili.
 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya, Sophia Kumbuli akisisitiza jambo kuhusiana na tukio hilo.

Wananchi na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Na JamiiMojaBlog
Jeshi la Polisi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya linamshikilia muuguzi wa afya katika  hospitali ya Wilaya ya Chunya, Patricia Kisoti, kwa kutokana na uzembe uliopekekea mama mjamzito kujifungua mtoto akiwa amekufa.

Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa muuguzi huyo Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya  Rehema Madusa amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo nichakinyama  na kimetia aibu sekta ya afya.

Amesema September 4, mwaka huu katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, mjamzito huyo akiwa  ameongozana na mwenzake walifika kituoni hapo usiku, wakihitaji huduma ya haraka kutokana na hali ya mgonjwa kuwa mbaya.

Amesema licha ya mama huyo kufika akiwa katika hali mbaya alijitahidi kujieleza ili apate huduma kwa waaguzi waliokuwa zamu akiwemo mtuhumiwa huyo Patricia Kisoti ambaye ndiye aliyetakiwa kumhudumia mgonjwa huyo lakini alishindwa kutoa ushirikiano badala yake alitoa majibu ya kejeli na kushindwa msaada wowote.

Amesema kama mama huyo angemshughulikiwa kwa haraka ikiwa na muuguzi huyo kutoa taarifa kwa ngazi za juu baada ya kuona tatizo hilo haliwezi, basi mtoto huyo angekuwa hai.

Aidha, Mkuu huyo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya, Sophia Kumbuli kuhakikisha anachukua hatua za kinidhamu kwa wahusika wote.

Amesem kifo cha kichanga hicho, kwa asilimia kubwa  kilitokana na uzembe wa muuguzi huyo kutokana na maalezo yaliyotelewa mgonjwa huyo.

Akizungumzia sakata hilo, Maria Solomoni, amesema  siku hiyo, yeye akiwa ameongozana na mwenzake aliyemtambulisha kuwa alikuwa ni wifi yake, walifika katika kituo hicho cha afya majira ya usiku, huku akiwa ameshikwa na uchungu, ambapo waligonga mlango wa chumba cha nesi ambao kwa muda huo ulikuwa umefungwa.
Maria, aliendelea kufafanua kuwa aliendelea kuteseka na mates ohayo mpka majira ya saa kumi namoja alifajili ndipo alipoona wanaume wawili wakimuhangaikia na kumuingiza katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa oparesheni.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani, alikiri kutokea kwa tukio hilo kituoni hapo na kwamba katika uchunguzi wao wa awali umebaini kwamba katika tukio lililomkuta Maria Solomoni, ndani yake kulikuwa na uzembe.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA MBEYA ATIWA MBARONI KWA MADAI AMESABABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA
MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA MBEYA ATIWA MBARONI KWA MADAI AMESABABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhX9fAK1xbvbyBPTCYv_wuBGBTnWmAVCoCbwwzQaAoMVJ6Edc_NZcz87zpyWwszvCzumINIZoJQyiqJrU5YzIcDd3jXtxJkKF7O3I126hPdJkhepPwVFgsiZ47-Qk2zSqIpnHfbbSobrIMy/s640/DSC_0758.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhX9fAK1xbvbyBPTCYv_wuBGBTnWmAVCoCbwwzQaAoMVJ6Edc_NZcz87zpyWwszvCzumINIZoJQyiqJrU5YzIcDd3jXtxJkKF7O3I126hPdJkhepPwVFgsiZ47-Qk2zSqIpnHfbbSobrIMy/s72-c/DSC_0758.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/muuguzi-hospital-ya-wilaya-ya-mbeya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/muuguzi-hospital-ya-wilaya-ya-mbeya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy