POLISI YATOA ONYO WANAOIBIA WATALII ZANZIBAR
Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Hasina Tawfiqi wakati wa Operesheni maalum ya kukabililiana na mtandao wa dawa za kulevya na uhalifu dhidi ya watalii inayoendelea katika mikoa ya Zanzibar. (Picha na Jeshi la Polisi)
HomeJamii

POLISI YATOA ONYO WANAOIBIA WATALII ZANZIBAR

Na Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi nchini limesema Operesheni ya kukabiliana na mtandao wa dawa za kulevya katika Visiwa vya Zanzibar...




Na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limesema Operesheni ya kukabiliana na mtandao wa dawa za kulevya katika Visiwa vya Zanzibar itaendelea sambamba na kuwadhibiti wahalifu wanaofanya vitendo vya kuwaibia na kuwadhuru watalii jambo ambalo linatia doa usalama uliopo katika visiwa hivyo.
Kauli hiyo imetolewa  na Mkuu wa Operesheni maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas ambaye yupo Zanzibar akiongoza timu iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Kamisheni ya Polisi Zanzibar kwa lengo la kuongeza nguvu katika kuzuia na kupambana na mtandao wa dawa za kulevya pamoja na uhalifu dhidi ya watalii.
DCP Sabas amesema Operesheni hiyo haitawaacha wahalifu hao salama kwa kuwa inafanyika kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa haiachi mhalifu yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo viovu ambavyo vimekuwa vikichafua taswira nzuri ya usalama.
“Operesheni hii ni endelevu na niwape tu salamu wahalifu kuwa jambo la msingi ni wao wenyewe kujisalimisha kwa kuwa awamu hii hata wakikimbia tutawasaka na kuwakamata  kwa kuwa nguvu ipo na tunapata ushirikiano kwa wananchi wema wanaochukia vitendo vya uhalifu” Alisema Sabas.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi Hasina Tawfiqi amesema katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Heroin jumla ya Kete 695 sawa na ujazo wa gramu 31.3 pamoja na Watuhumiwa 21.

Amewasihii wakazi wa Kaskazini Unguja na mikoa jirani kuendelea kutoa taarifa ili kuweza kukomesha mtandao wa biashara hiyo pamoja na kuhakikisha kuwa watalii wanaotembelea mkoa huo wanafanya kazi zao kwa amani na usalama.
Operesheni hiyo pia imefanyika katika Mkoa wa Mjini magharibi ambapo Jumla ya watuhumiwa 58 walikamatwa pamoja na dawa za kulevya aina heroin Kete 1293 na Vifuko vitatu sawa na Gramu 74.385.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: POLISI YATOA ONYO WANAOIBIA WATALII ZANZIBAR
POLISI YATOA ONYO WANAOIBIA WATALII ZANZIBAR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjcVpM6J3yvbsFjvvKaQgvZJW-NxlQrNbnu0s6ulbcu9qx7JYu0L9MMc47nbwFhulFDqFkIr9EGbOnDmbRTLOngXEuuPFwBJBvz74Dk4QMN4nkAa5cA65C5puVDPwsNmU1JEhq01vxHSWE/s640/Mkuu+wa+Operesheni+Maalum+za+Polisi%252C+Naibu+Kamishna+wa+Polisi+DCP+Liberatus+Sabas.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjcVpM6J3yvbsFjvvKaQgvZJW-NxlQrNbnu0s6ulbcu9qx7JYu0L9MMc47nbwFhulFDqFkIr9EGbOnDmbRTLOngXEuuPFwBJBvz74Dk4QMN4nkAa5cA65C5puVDPwsNmU1JEhq01vxHSWE/s72-c/Mkuu+wa+Operesheni+Maalum+za+Polisi%252C+Naibu+Kamishna+wa+Polisi+DCP+Liberatus+Sabas.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/polisi-yatoa-onyo-wanaoibia-watalii.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/polisi-yatoa-onyo-wanaoibia-watalii.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy