OIF YAELEZEA FURSA ZILIZOPO KWA WATANZANIA WANAOJUA KIFARANSA
HomeJamii

OIF YAELEZEA FURSA ZILIZOPO KWA WATANZANIA WANAOJUA KIFARANSA

Shirika la Kimataifa la La Francophonioe (OIF) ambalo linajumuisha nchi 84 ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa limesema kwamba ni muh...

RAIS DKT. MAGUFULI ATIA SAINI NYARAKA ZA MSAMAHA WA WAFUNGWA 63 AMBAPO 61 WALIKUWA WA KUNYONGWA NA MAJINA MAWILI (2) YA WAFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA.
RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU MJINI DODOMA LEO
UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA




Shirika la Kimataifa la La Francophonioe (OIF) ambalo linajumuisha nchi 84 ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa limesema kwamba ni muhimu kwa Watanzania kujifunza lugha ya Kifaransa kwa sababu kuna fursa nyingi wanaweza kuzipata kwa kuzungumza lugha hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25, Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier amesema katika nchi hizo kuna nafasi za kazi nyingi ambazo kama Watanzania watajifunza Kifaransa wanaweza kuzipata.

Alisema Tanzania inazungukwa na nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa kama Burundi, Jumhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na hivyo kwa wananchi wa Tanzania hiyo ni fursa ambayo wanaweza kuitumia katika shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.
Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier akizungumza kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25.

"Hapa Tanzania wanazungumza Kiswahili na baadhi ya lugha za nje na hili linafungua milango ya ajira ndani ya Tanzania na nje ya nchi kwa wanaozungumza Kifaransa na ndiyo maana tunatangaza lugha hii ili watu waitumie."

"Tanzania inapakana na nchi nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa hivyo ni muhimu Kifaransa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu kwa manufaa ya Watanzania ambao wanatamani kupata nafasi katika nchi zinazozungumza Kifaransa," alisema Clavier.

Aidha, Clavier alizungumzia Wiki ya Francophonioe na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika maonesho mbalimbali yaliyoangaliwa na OIF ambayo yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa, Allience Française, Century Cinemax ya Oysterbay na Jakaya Kikwete Omnisport Park iliyopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: OIF YAELEZEA FURSA ZILIZOPO KWA WATANZANIA WANAOJUA KIFARANSA
OIF YAELEZEA FURSA ZILIZOPO KWA WATANZANIA WANAOJUA KIFARANSA
http://dewjiblog.co.tz/wp-content/uploads/2018/03/DSC_0185.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/oif-yaelezea-fursa-zilizopo-kwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/oif-yaelezea-fursa-zilizopo-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy