MKURANGA, KIBITI, IKWIRIRI, ZAANZA KUPATA UMEME WA GRIDI
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha kupoza umeme cha Mbagala kilichopo jijini Dar es Saalam tarehe 22 Machi, 2018. Kulia ni Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Alex Adam


HomeJamii

MKURANGA, KIBITI, IKWIRIRI, ZAANZA KUPATA UMEME WA GRIDI

Na Greyson Mwase, Pwani Machi 23, 2018 Wilaya za Mkuranga, Kibiti na wilaya ya Rufiji katika kata ya  Ikwiriri zimeanza kupata nishat...

MAHAFALI YA 11 YA CHUO KIKUU ARDHI (ARU) YAFANA DAR ES SALAAM
WAZIRI MHAGAMA AKABIDHIWA VIFAA VYA WATU WENYE ULEMAVU CHUO CHA UFUNDI CHA YOMBO IKIWA NI MSAADA KUTOKA SERIKALI YA KUWAIT
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA

Na Greyson Mwase, Pwani
Machi 23, 2018
Wilaya za Mkuranga, Kibiti na wilaya ya Rufiji katika kata ya  Ikwiriri zimeanza kupata nishati ya uhakika ya umeme mara baada ya kuunganishwa katika Gridi ya Taifa na kukamilika kwa kituo cha kupozea umeme cha Mbagala kilichopo jijini Dar es Salaam.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati akizungumza na wananchi wa Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani katika ziara yake ya siku moja jana (tarehe 22 Machi, 2018) ya kukagua miundombinu ya umeme iliyounganishwa na Gridi ya Taifa kutokea katika kituo cha kupoza umeme cha Mbagala hadi Ikwiriri na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Dkt. Kalemani alisema lengo la kuunganisha wilaya hizo na Gridi  ya taifa ni kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya umeme wa uhakika na kuondokana na umeme unaotokana na mitambo ya mafuta ya Somangafungu  ambayo imekuwa ikiharibika mara kwa mara.
Alisema awali kabla ya wilaya hizo kuunganishwa na Gridi ya Taifa, kulikuwepo na changamoto ya kukatika kwa umeme katika wilaya hizo kutokana na mitambo kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali iliamua kuunganisha  wilaya hizo kwenye Gridi ya Taifa ili kuwepo na umeme wa uhakika ambao mbali na matumizi ya majumbani unategemewa na viwanda  vilivyopo katika mkoa wa Pwani
Katika hatua nyingine akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinyanya kilichopo katika wilaya ya Kibiti mkoani Pwani ambapo aliwasha rasmi umeme, Waziri Kalemani aliwataka wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kupitia REA kuhakikisha vijiji vyote na  vitongoji vyake vinapata umeme wa uhakika.
Aliwataka wakandarasi hao kuhakikisha sehemu za huduma muhimu za jamii kama vile vituo vya afya, shule, kanisa na misikiti zinapata umeme wa uhakika.
Waziri Kalemani pia aliwataka wananchi kuanza kutandaza mifumo ya umeme (wiring) majumbani pamoja na kulipia shilingi 27,000 kwa ajili ya kuunganishiwa na huduma ya umeme.
Alielekeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha umeme haukatiki na kufungua ofisi karibu na wananchi ili kuepuka adha ya wananchi kwenda mbali kufuata huduma ya kuunganishiwa umeme.
“ TANESCO ni lazima mhakikishe mnawafuata wananchi na kukusanya  fedha kwa ajili ya kuunganishiwa na huduma ya umeme, hata kama ni chini ya mwembe badala  ya wananchi kutumia gharama kubwa kwenda mjini kuwafuata,” alisema Dkt. Kalemani
Wakati huohuo wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa kijiji hicho waliishukuru  Serikali kwa kuwafikishia huduma ya umeme na kuongeza kuwa uchumi wa wilaya ya Kibiti utaanza kukua kutokana na ajira kuongezeka.
Hamisi Mkwera akizungumza kwa  niaba ya wananchi wenzake alisema uwepo wa umeme wa uhakika kwenye  wilaya yao utachochea ukuaji wa viwanda na kuongezeka kwa fursa za ajira kwa wakazi waishio karibu na viwanda husika



Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Alex Adam (wa pili kushoto) akielezea shughuli zinazofanywa na kituo cha kupoza umeme cha Mbagala kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) katika ziara hiyo.

Mafundi wa kampuni ya Sengerema Engineering wakikamilisha ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa ajili ya kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa katika kijiji cha Kinyanya kilichopo wilayani Kibiti mkoani Pwani.



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akibonyeza kitufe kuashiria uwashaji wa umeme katika kijiji cha Kinyanya kilichopo wilayani Kibiti mkoani Pwani.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKURANGA, KIBITI, IKWIRIRI, ZAANZA KUPATA UMEME WA GRIDI
MKURANGA, KIBITI, IKWIRIRI, ZAANZA KUPATA UMEME WA GRIDI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjnnfVrlDKsmzH-iBxthQJjBEuJbopbxDnWURoySXYVvkWq3W_LXapTkDegg2-1uxVp8oWv6t8j0M6DfEGSgMmim-q44ahx1dwi1fTCQdZrCjTIwWbidHOtEDAn9861CtMflSUpcrTswmk/s640/PICHA+NA+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjnnfVrlDKsmzH-iBxthQJjBEuJbopbxDnWURoySXYVvkWq3W_LXapTkDegg2-1uxVp8oWv6t8j0M6DfEGSgMmim-q44ahx1dwi1fTCQdZrCjTIwWbidHOtEDAn9861CtMflSUpcrTswmk/s72-c/PICHA+NA+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mkuranga-kibiti-ikwiriri-zaanza-kupata.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mkuranga-kibiti-ikwiriri-zaanza-kupata.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy