WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU
HomeJamii

WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii irudi kwenye maeneo yote yenye migogoro ya mipaka na iungane na Halmash...

TAHADHALI YA UWEPO WA UKAME WA CHAKULA
WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA 6 WA WADAU WA NSSF
BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LAJADILI MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii irudi kwenye maeneo yote yenye migogoro ya mipaka na iungane na Halmashauri za wilaya ili waweze kutoa majibu kwa wananchi.


Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 8, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Urambo, Margaret Sitta wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma.


Bibi Sitta alitaka kujua Serikali imeweka taratibu na mikakati gani ya kumaliza migogoro ya mipaka inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya hifadhi za misitu nchini kwa kuwa wananchi wanahitaji maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na mifugo.


Waziri Mkuu amesema Serikali iliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iweke vigingi kwenye maeneo yote yanayozunguka hifadhi za misitu ili kuweka alama zitakazopunguza migogoro ya kuingiliana kati ya wananchi walioko kwenye vijiji na wahifadhi kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu hiyo.


Amesema maagizo hayo yalitolewa baada ya kugundua kuwa kuna migogoro mingi kati ya wananchi walioko katika vijiji vya jirani na misitu iliyohifadhiwa kisheria ambayo ina ramani.


“Lakini tunatambua kwamba wanapoendelea na zoezi hilo la uwekaji alama, inaweza kutokea kijiji kikajikuta kipo ndani ya mipaka ya hifadhi na inaweza kusababisha kutoelewana kati ya wanakijiji na wenye mamlaka ya hifadhi.”


“Tuliwasihi wanakijiji wakati zoezi hili linaendelea na hata kama kijiji kitajikuta kimezungukwa na hizo alama, wanakijiji watulie ili kazi ya awali ikamilike na pale kwenye mgogoro, Serikali itarudi tena kuja kuangalia mgogoro huo na kufanya tathmini ya kina.”


Amesema Serikali iliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii inapofanya kazi hiyo ya kuweka vigingi lazima ishirikishe mamlaka za halmashauri na kijiji husika na wao washiriki katika zoezi hilo ili kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima.


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaielekeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi izitumie ranchi za NARCO na kugawa katika vitalu ili kubaini ukubwa wa eneo iliyonayo ndipo iweze kufanya uamuzi wa kugawa vitalu hivyo kwa wafugaji.


Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Nkenge, Balozi Dkt. Diodorus Kamala aliyetaka kujua taarifa ya kamati iliyoundwa na Serikali kufuatilia migogoro ya ranchi zilizokuwa chini ya NARCO na wafugaji, itapelekwa lini bungeni ili iweze kujadiliwa.


Waziri Mkuu amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliunda tume ya kufuatilia maeneo yote ya ranchi za Taifa na kuyapima maeneo hayo lakini pia kujua ni akina nani wanayamiliki maeneo hayo, kubaini kama walipewa kihalali, na kama ni kweli wanamiliki mifugo yoyote kwenye maeneo tajwa.


Kuhusu kupelekwa bungeni kwa taarifa ya tume hiyo, Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Mifugo aikamilishe na kuiwasilisha Bungeni kama taratibu zinavyotaka ili kuwawezesha wabunge na wananchi wajue dira na mwelekeo wa Serikali wa namna ya kufuga mifugo hiyo kwa njia ambazo zitawaletea tija lakini kikubwa zaidi ni kumaliza migogoro baina ya wakulima na wafugaji.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, FEBRUARI 8, 2018.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU
WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8J_tZ18SizaitUT4ER0DHZ10xXYPzAFcdwqER67qDMaIBSrBOHNXAqZY9UFMomrWy-LKbuxiMb6uCshwEW8Vs2CXmnguwUI6QjT2pn-uH139wtti3lfY73zXGWN2DiJPowcfRo8wwznd-/s320/PMO_7868-768x587.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8J_tZ18SizaitUT4ER0DHZ10xXYPzAFcdwqER67qDMaIBSrBOHNXAqZY9UFMomrWy-LKbuxiMb6uCshwEW8Vs2CXmnguwUI6QjT2pn-uH139wtti3lfY73zXGWN2DiJPowcfRo8wwznd-/s72-c/PMO_7868-768x587.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/wizara-ya-maliasili-yaagizwa-irudi-kwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/wizara-ya-maliasili-yaagizwa-irudi-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy