UDART YAINGIZA NCHINI MABASI MAPYA 70 KUONGEZA NGUVU YA USAFIRISHAJI ABIRIA DAR ES SALAAM
HomeJamii

UDART YAINGIZA NCHINI MABASI MAPYA 70 KUONGEZA NGUVU YA USAFIRISHAJI ABIRIA DAR ES SALAAM

 Maofisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) wakishuhudia wakati mabasi ya Kampuni  ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar e...

WAZIRI KAIRUKI AELEKEZA MTUMISHI ALIYEHAKIKIWA KWA CHETI TOFAUTI NA MAJINA ANAYOLIPWA MSHAHARA KUONDOLEWA KWENYE PAYROLL
VIJANA DAR ES SALAAM WAANZA MASOMO YA TEHAMA
MWANAHABARI WA ITV SPENCER LAMECK ALIVYOUAGA UKAPERA KTK KANISA LA TAG KINONDONI REVIVAL CHURCH DAR




 Maofisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) wakishuhudia wakati mabasi ya Kampuni  ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam (UDART) yalipokuwa yakishushwa kutoka katika meli jijini Dar es Salaam leo hii asubuhi. Jumla ya mabasi 70 yalipokelewa.
 Sehemu ya kupita mabasi hayo ikiandaliwa wakati wa ushushaji wake kutoka katika meli ya Kichina.
 Moja ya mabasi hayo likitoka katika meli.
 Moja kati ya mabasi hayo likiwa limetoka katika meli.
Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Charles Newe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea mabasi hayo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam (UDART), imeingiza nchini mabasi mapya 70 kutoka China kwa ajili ya kuongeza nguvu ya usafirishaji abiria.

Akizungumza wakati wa upokeaji wa mabasi hayo Bandarini jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Charles Newe alisema hiyo ni hatua nzuri kwa kampuni hiyo yenye lengo la uhakika wa kutoa huduma bora ya usafiri kwa abiria jijini.

Alisema mabasi hayo yataongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria hivyo kuwapunguzia adha ya usafiri wakati wa jiji la Dar es Salaam.

Alisema mabasi hayo yataongeza uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa wananchi na kupunguza gharama ya usafiri ambapo kwa wale wenye magari wataacha kuyatumia magari yao kwenda kazini ambapo wataokoa sh.8000 katika kila sh.10000 waliyokuwa wakiitumia kwa siku kununulia mafuta.

"Wenye magari sasa hivi watakuwa wanaokoa sh.8000 kila siku ambapo watakuwa wakitumia mabasi yetu kwa sh.2000 tu kuja kazini na kurudi majumbani kwao" alisema Newe.

Alisema kiasi hicho cha fedha kitakachookolewa kitaweza kwenda kufanya shughuli zingine za maendeleo ya nchi na mtu mmoja mmoja.

Akizungumzia mabasi hayo alisema yanauwezo wa kubeba watu kuanzia 150 hadi 160 na kuwa bei ya basi moja ni limenunuliwa kwa dola za Marekani 260,000 na kuwa mabasi hayo yanafikisha idadi ya mabasi 210 huku mahitaji ya mabasi hayo ikiwa ni 305 kwa awamu ya kwanza.

Alisema changamoto kubwa iliyokuwepo ni uchache wa mabasi yaliyokuwepo ambapo watu walilazimika kupanda kwa wingi lakini kwa ongezeko la mabasi hayo itasaidia kupunguza changamoto hiyo.


(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UDART YAINGIZA NCHINI MABASI MAPYA 70 KUONGEZA NGUVU YA USAFIRISHAJI ABIRIA DAR ES SALAAM
UDART YAINGIZA NCHINI MABASI MAPYA 70 KUONGEZA NGUVU YA USAFIRISHAJI ABIRIA DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhn1UFSxxRtu0b73FSX0xgpHbVR-n-H3882k6ZXcY7AQxx3sgG8DMNGGW05ReScMVhPwfk6YKjJKdX-bIYE5nhu4CmnRmtAvn4-KHx9FhioEPPQpDGP_F5q_v1dNfJp1qvH-pf9KhETZtgw/s640/IMG_0953.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhn1UFSxxRtu0b73FSX0xgpHbVR-n-H3882k6ZXcY7AQxx3sgG8DMNGGW05ReScMVhPwfk6YKjJKdX-bIYE5nhu4CmnRmtAvn4-KHx9FhioEPPQpDGP_F5q_v1dNfJp1qvH-pf9KhETZtgw/s72-c/IMG_0953.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/udart-yaingiza-nchini-mabasi-mapya-70.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/udart-yaingiza-nchini-mabasi-mapya-70.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy