TIGO YAZINDUA KAMPENI MPYA YA NYAKA NYAKA BONUS

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Dar es Salaam leo katik...



Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus ambapo wateja wa Tigo wanapata bonasi ya hadi GB 1 ya data pamoja na nafasi ya kushinda simu janja ya 4G aina ya TECNO R6 kila saa wanaponunua bando za intaneti kupitia namba *147*00# . Katikati ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf pamoja na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kulia).


Bonasi Kemkem Kwa Wateja Wa Tigo Watakaonunua Bando Kupitia *147*00#  Pata hadi GB 1 bure na nafasi ya kushinda simu janja ya 4G kila saa!

Dar es Salaam, Februari 9, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni murwa kwa wateja wake wote watakaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#,  ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter.

Pamoja na haya, wateja hao pia watapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zaidi ya elfu moja ambazo zinatolewa na Tigo katika promosheni hiyo kabambe ya ‘Nyaka Nyaka Bonus’.

Akitangaza ofa hizo jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik Boudiaf alisema kuwa ofa hizo murwa ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaolenga kukutana na mahitaji ya wateja na kuwezesha kila mtu afurahie huduma za kidigitali katika mtandao ulioboreshwa wa Tigo.

“Kupitia mtandao wetu mathubuti wa 4G wateja wetu tayari wanafurahia huduma bora zaidi za intaneti. Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inatoa fursa kubwa kwa wateja wengi zaidi kumiliki simu janja zenye uwezo wa 4G na kupokea bonasi kubwa za data zitakazowawezesha kuwa sehemu ya mageuzi makubwa ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ alisema.

Tigo ndio mtandao unaoelewa zaidi mahitaji ya wateja wake ambapo katika soko la simu za mkononi nchini, ni wateja wa Tigo pekee wanaopokea bonasi za bure kwa kila kifurushi wanachonunua. Tigo pia imejizolea umaarufu mkubwa kwa promosheni zake bunifu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema kupitia promosheni mpya ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inalenga kuongeza matumizi ya data pamoja na kuongeza matumizi ya simu janja za kisasa (Smartphone) nchini, hivyo kuisogeza Tanzania hatua moja mbele zaidi katika ulimwengu wa kidigitali.

‘Tunafahamu kuwa idadi kubwa ya Watanzania bado hawajafikiwa na huduma za mtandao na ndio maana Tigo inazidi kuwekeza katika kupanua na kuboresha huduma zake za mtandao. Kupitia promosheni hii tunalenga kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini,’ alisema.


“Tunawakaribisha wateja wetu wote kuchangamkia fursa hii kwa kununua vifurushi vya data vya kuanzia TZS 1,000 kupitia menu yetu ya *147*00#  ili waweze kufaidi bonasi za papo hapo za intaneti kwa matumizi ya mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Vile vile, kila kifurushi wanachonunua kitawaingiza katika droo ambapo watapata nafasi ya kushinda mojawapo za zaidi ya simu janja 1,000 aina ya TECNO R6 yenye uwezo wa 4G ambazo Tigo inatoa katika msimu huu,” Tarik alisisitiza.  

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIGO YAZINDUA KAMPENI MPYA YA NYAKA NYAKA BONUS
TIGO YAZINDUA KAMPENI MPYA YA NYAKA NYAKA BONUS
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzwevvHKCJ27D_pB8eOdAkn6q_qutiXzREZ9wTrPu5nPGWrj6oGT9-s_vSG0cccXlU8JAKUq5TLsBwlTJhEq8AW7oDJ5CEJFWiZv1l0HlTHRjxhNGPL6Sd92v-uKClmbGSXab7TnEI7Ek/s640/ot+pic-0110.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzwevvHKCJ27D_pB8eOdAkn6q_qutiXzREZ9wTrPu5nPGWrj6oGT9-s_vSG0cccXlU8JAKUq5TLsBwlTJhEq8AW7oDJ5CEJFWiZv1l0HlTHRjxhNGPL6Sd92v-uKClmbGSXab7TnEI7Ek/s72-c/ot+pic-0110.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/tigo-yazindua-kampeni-mpya-ya-nyaka.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/tigo-yazindua-kampeni-mpya-ya-nyaka.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy