TAKUKURU TANGA YAPOKEA TAARIFA 204 ZA VITENDO YA RUSHWA
HomeJamii

TAKUKURU TANGA YAPOKEA TAARIFA 204 ZA VITENDO YA RUSHWA

  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwez...

MFUMO WA MANUNUZI YA UMEME KUPITIA LUKU KUZIMWA JUMAPILI HII
JARIDA LA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU - FEBRUARI, 2017
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUTA AGIZO LA KUFUNGA NDOA KWA SHARTI LA KUWA NA CHETI CHA KUZALIWA
 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher
Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba
mwaka 2017.




 Sehemu ya waandishi wa habari
wakichukua matukio


 Sehemu ya wanahabari
mkoani Tanga wakifuatilia matukio katika mkutano huo




TAASISI ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tanga (Takukuru) imepokea taarifa 204 za
vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi wakizilalamikia idara mbalimbali za
serikali na sekta binafsi.




Hayo yalibainishwa
na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za
utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba
mwaka 2017.




Alisema taarifa
hizo ni ongezeko la taarifa 30 sawa na asilimia 17 ukilinganisha
 na kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo
taarifa zilizo pokelewa ni 174.




Aidha alisema
katika taarifa hizo 52 zilihusu serikali za mitaa, ardhi/ mabaraza ya
ardhi 33,vyama
vya siasa 28,Polisi 23,Elimu 18,Mahakama 16,Afya 15,Kilimo 8,Tasaf 5,Bandari
(TPA) 1,Maji 1,Ushirika 1,Uhamiaji 1,Tanesco 1 na Misitu
1.




Mkuu huyo
alisema kati ya taarifa hizo 204 zilizopokelewa taarifa 92 zinaendelea
kuchunguzwa wakati nyengine 66 uchunguzi wake ulikamilika na majalada kufungwa
kutokana na kukosekana kwa ushahidi.




Aliongeza kuwa
taarifa 46 zilihamishwa kwenye idara nyengine kwa sababu zilikuwa zikihusiana
na makosa chini ya kuzuia na kupambana na
rushwa.




Hata hivyo
alisema katika uendeshaji wa mashitaka takukuru mkoa wa Tanga imefanya
uendeshaji wa kesi 18 mahakamani ambapo kati ya kesi hizo 9 zilifunguliwa
kipindi cha Julai 2017 hadi Desemba 2017 na kesi 9 ni za kabla ya
Julai 2017.




Alieleza pia
katika kipindi hicho usikilizwaji wa kesi moja huko wilayani Lushoto kwa
mshtakiwa aliyejulikana kwa jina la Ally Mgovi ambaye alikuwa Afisa Mtendaji wa
Kijiji cha Funta ambapo alifikishwa mahakamani kwa makosa ya ubadhirifu wa
pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa ajili ya
wakulima.




Alisema
mshtakiwa huyo alipatikana na hatia alihukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka
mitatu au kulipa faini ya Tsh Milioni 1.9 ambapo alishindwa kulipa faini hivyo
alipelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka
mitatu.




Akizungumzia fedha
ambazo zimeokolewa na kazi za uchunguzi na udhibiti ambapo katika utekelezaji
wa majukumu yao kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2017 kumekuwa na ongezeko la
fedha walizookoa na kuzirejesha serikalini kutoka milioni 6,450,000 kwa miezi
sita ya mwanzo hadi Milioni 52,508,260.




Alieleza fedha
hizo zilikuwa kwa ajili ya malipo ya wanafunzi hewa ndani ya mpango wa elimu
bila malipo katika shule za sekondari,mishahara hewa na gharama kwa ajili ya
semina hewa. (Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga
Raha)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAKUKURU TANGA YAPOKEA TAARIFA 204 ZA VITENDO YA RUSHWA
TAKUKURU TANGA YAPOKEA TAARIFA 204 ZA VITENDO YA RUSHWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNvbf6LI-uInNyj5QCRsiWyCxv_S9MMF6EEji_nCZYlbDCAj36BQj3fw0BpZ_m39LSJnVW5vcP1UT2mLByEcAkLCwe5O1Wan5vZ-1fwDhZe228w_IQaC4Q_-SFMdJtyTG4wMnqhjKigDDt/s640/_MG_1977.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNvbf6LI-uInNyj5QCRsiWyCxv_S9MMF6EEji_nCZYlbDCAj36BQj3fw0BpZ_m39LSJnVW5vcP1UT2mLByEcAkLCwe5O1Wan5vZ-1fwDhZe228w_IQaC4Q_-SFMdJtyTG4wMnqhjKigDDt/s72-c/_MG_1977.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/takukuru-tanga-yapokea-taarifa-204-za.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/takukuru-tanga-yapokea-taarifa-204-za.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy