Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa Mamlaka ya Viwanja Ndege Nchini (TAA), kukusanya ...
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa Mamlaka ya Viwanja Ndege Nchini (TAA), kukusanya fedha za madeni ambayo inadai kutoka kwa watoa huduma mbalimbali katika viwanja vyote vya ndege ili ziweze kutumika kuendeleza miundombinu.
Kauli hiyo ametoa jijini Mwanza, baada kukagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja cha ndege na hali ya uendeshaji katika kiwanja hicho ambapo amebaini kuwa kuna madeni ambayo yanaweza kulipika na kuweza kurahisisha shughuli za kiuendeshaji ikiwemo kujenga uzio ili kuongeza usalama kiwanjani hapo.
"Nataka TAA mkusanye madeni yote mnayodai, fedha hizi zikipatikana zinaweza kutumika kujenga uzio kwa ajili ya kulinda usalama wa uwanja ili wananchi wasiweze kuvamia na pia usalama wa ndege zinazoruka na kutua", amesisitiza Prof. Mbarawa.
Amefafanua kuwa kama Taasisi hizi zikikusanya madeni na watoa huduma wakalipa kodi kwa wakati kutasaida Serikali kuboresha maendeleo ya miundombinu.
Kuhusu maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho. Prof. Mbarawa amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi ambapo kwa sasa umefikia asilimia 60.
Ameongeza kuwa ujenzi huo unategemewa kumalizika mwezi Julai mwaka huu na utagharimu kiasi cha shilingi takribani bilioni 94.
Aidha amesema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria mara miradi inayoendelea kukamilika.
Naye Msimamizi wa Kiwanja hicho ambaye ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mwanza, Mhandisi Joseph Mwami, amesema kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa jengo la kuongoza ndege, eneo la maegesho na njia za kuruka na kutua ndege
Mhandisi Mwami, amefafanua kuwa njia ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja hicho imeongezwa urefu wa mita 500 ili kuifanya kufikia urefu wa KM 3.5 ili kuwezesha ndege kubwa za kimataifa kuweza kutua na kuruka katika kiwanja hicho.
Katika hatua nyingine Waziri Prof Mbarawa amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa barabara ya Mwaloni-Pasiansi-Airport yenye urefu wa KM 5.3 kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi mei mwaka huu na utagharimu kiasi cha shillingi bilioni 9.5.
"Nimekagua na niwapongeze Kampuni ya wazawa ya Nyanza Road kwa kazi nzuri mliyofanya katika ujenzi kwa barabara hii", amesema Prof Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kutunza na kulinda miundombinu hiyo kwa manufaa ya kuongeza tija na maendeleo kwao kwan inapunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa na Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kugharamia utekelezaji wa miradi hiyo.
Waziri Prof Mbarawa yuko mkoani mwanza kwa ziara ya siku akiwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miundombinu ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi barabara ya Pasiansi hadi Airport KM 4.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mwanza.
|
Muonekano wa sehemu ya barababara ya Pasiansi hadi Airport KM 4.6, inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mwanza.
|
Muonekano wa eneo la kuegesha ndege ambalo ni moja ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi na uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza.
|
COMMENTS