JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA Tele: +255 0262322761-5 Fax No. +2550262324218 Email: cna@bunge.go.tz ...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
| ||
Tele: +255 0262322761-5
Fax No. +2550262324218
Email: cna@bunge.go.tz
|
Ofisiya Bunge
S.L.P 941
DODOMA
| |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru kufuatia kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 2 Februari 2018, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
![]() |
| Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru enzi za uhai wake. |
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, natoa pole kwa familia ya marehemu na Watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza mwanasiasa Mkongwe katika nchi hii ambaye licha ya kuwahi kuwa Mbunge lakini pia ameitumikia Serikali katika nyadhifa mbalimbali,” alisema.
“Binafsi nilifanya kazi kwa karibu na Mzee Kingunge wakati wa Bunge letu na pia kwenye Bunge la Katiba ambapo tulikuwa wote kamati namba nane nikiwa Mwenyekiti wake, mchango wake ulitusaidia sana” aliongeza Mheshimiwa Spika.
Mheshimiwa Spika amemuomba Mwenyezi Mungu awape subira, nguvu na faraja familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kupotelewa na mpendwa wao.
Imetolewa na: Ofisi ya Spika
S.L.P. 941
DODOMA
02 Februari 2018


COMMENTS