PROF. KAMUZORA ATEMBELEA NA KUKAGUA KITUO CHA OPARESHENI NA MAWASILIANO YA DHARURA.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akisaini kitabu cha wageni alipoenda kukagua kituo cha Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali pembeni ni Kamanda wa Jeshi la zimamoto kanda maalumu Afande Peter Mabusi. Kituo hicho kipo  Ofisi ya kanda Maalumu ya jeshi la Zimamoto  jijini Dar es Salaam.

HomeJamii

PROF. KAMUZORA ATEMBELEA NA KUKAGUA KITUO CHA OPARESHENI NA MAWASILIANO YA DHARURA.

Na. Mwandishi Wetu. Katibu mkuu (Sera na Uratibu)  Prof. Faustin Kamuzora  ametembelea na kukagua kituo cha operesheni ya mawa...

BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA VUAI ALI VUAI
WCF TELLS EMPLOYERS: PAY CONTRIBUTIONS AS PER THE LAW
IGP SIMON SIRRO AANZA KAZI, AZUNGUMZIA MKAKATI WA KUTOKOMEZA MAUAJI KIBITI




Na. Mwandishi Wetu.
Katibu mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora ametembelea na kukagua kituo cha operesheni ya mawasiliano ya dharura na kujua maendeleo ya kituo hicho kilichopo Ofisi ya kanda Maalumu ya jeshi la Zima moto Jijini Dar es Salaam.
Akitoa maelezo ya jinsi mradi huo unavyofanya kazi, Mratibu wa Taifa wa Mradi huo Alfei Daniel, alisema Mradi huo unafuatilia dharura za maafa nchini ikiwemo Ukame na Mafuriko umefadhiliwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani UNDP, ambapo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za maafa na vyanzo vyake, kuchambua taarifa hizo, kuhamasisha, kufuatilia, kutoa tahadhari za awali na kuratibu dharura katika ngazi ya kitaifa.
Alfei alifafanua kwamba, mradi huo una vituo 36 tofauti nchini ambavyo vina wawezesha kupata taarifa popote walipo kupitia mtandao maalumu, unaosaidia kutoa tahadhari kwa wananchi wa eneo linalotarajiwa kupata maafa, ambapo mpaka sasa mradi umechukua mabonde mawili yaani bonde la Pangani na bonde la mto Ruvuma.
“Mfumo ambao umefungwa unaweza kutabiri na kutoa taarifa za maafa zinazo weza kutokea popote katika vituo hivyo kwa kutumia mtandao, kwa mfano kujaa kwa maji ambako kuna weza kupelekea mafuriko. Mfumo huu ukikamilika utaweza kuonyesha ramani na vituo vyake vyote vya hali ya hewa.” Alisema Alfei.
Aidha baada ya kupata maelezo ya mradi huo Prof. Kamuzora alishauri mradi huo ufanye jitihada kutoa elimu ya uokoaji kwa wanafunzi mashuleni na raia wote kwa ujumla, na kwa watu wasiokua na elimu ya uokoaji watahadharishwe kukaa mbali na matukio ya maafa kwani wengi wao huathirika au kupoteza maisha katika uokoaji kwa kukosa elimu hiyo.
“Ni lazima uongozi uhakikishe matumizi mazuri ya rasilimali za mradi huu na kuzuia uharibifu wa vifaa na fedha zinazotelewa na mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali kuendesha mradi huu” Aliongeza Prof. Kamuzora.
Bw. Alfei alisisitiza kuwa mfumo huo unasaidia sana TMA katika kutabiri mabadiliko ya hali ya hewa kwa uhakika wa 87%, Wizara ya maji wanaweza kupata data kwa ajili ya kukuza vyanzo vya maji, vile vile hifadhi za taifa zinapata taarifa za hali ya hewa kwa urahisi kwa ajili ya kuhabarisha watalii na kujua mienendo ya wanyama, kwa ujumla huu mfumo unasaidia upatiknaji wa taarifa.
Mradi huu wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali ulianza rasmi mwezi Januari, 2017 kwa dhumuni hasa la kuwezesha mawasiliano ya kujitahadhari na maafa,kujiandaa na maafa, na kipindi cha maafa ambapo mawasialiana ya haraka huitajika ili kuokoa maisha na makazi ya watu. Hivyo mradi huu umeundwa ili kuwezesha mawasialiano ya saa 24 kwa siku saba za wiki.




Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na mifumo ya utolewaji wa tahadahri za awali Alfei Daniel jinsi mfumo unavyotumika kupata taarifa za hali ya hewa na tahadhari za maafa kutoka vituo mbalimbali nchini vilivyowekwa mfumo huo.





Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akitoa ushauri kwa Kamanda wa Jeshi la zimamoto Kanda Maalumu  Afande. Peter Mabusi na Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na mifumo ya utolewaji wa taadhari za awali Alfei Daniel namna ya kuboresha huduma zao na mradi huo.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PROF. KAMUZORA ATEMBELEA NA KUKAGUA KITUO CHA OPARESHENI NA MAWASILIANO YA DHARURA.
PROF. KAMUZORA ATEMBELEA NA KUKAGUA KITUO CHA OPARESHENI NA MAWASILIANO YA DHARURA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgN-NW1q-uwoH-_-uL6H5FWL8pzXvSQrr0hKQEueKezeGOfMzU-Zj-uYR-d2eOCz0-fvRrWFfg1OU6dp76x33tTMFanBTxbO7PPi_JUeiiOZ7vJ8_j6nT3FpV8WQfibtSnHiZVn-MoTBls/s640/IMG_0286.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgN-NW1q-uwoH-_-uL6H5FWL8pzXvSQrr0hKQEueKezeGOfMzU-Zj-uYR-d2eOCz0-fvRrWFfg1OU6dp76x33tTMFanBTxbO7PPi_JUeiiOZ7vJ8_j6nT3FpV8WQfibtSnHiZVn-MoTBls/s72-c/IMG_0286.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/prof-kamuzora-atembelea-na-kukagua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/prof-kamuzora-atembelea-na-kukagua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy