Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imetenga Shilingi bilioni thelathini (30...
Na Daudi
Manongi-MAELEZO, DODOMA
Serikali
kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imetenga Shilingi bilioni
thelathini (30) katika mwaka wa fedha 2017/2018 ili kukamilisha malipo ya fidia
kwa wananchi wa Kipunguni wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa ndege.
Hayo yamesemwa
leo na Naibu Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la
Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa.
“Ni kweli
Serikali ilifanya uthamini wa mali za wananchi ili kupisha upanuzi wa kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam mwishoni wa miaka ya 90 ambapo maeneo
yaliyoainishwa kwa ajili ya upanuzi huo ni Kipawa, Kigilagila na Kipunguni”, Alisema
Mhe. Ngonyani
Ameongeza kuwa
kutokana na gharama za fidia na uhaba wa fedha, Serikali imekuwa ikilipa fidia
kwa wakazi hao kwa awamu.
Ambapo Mwaka
2009/10 wakazi wapatao 1500 wa eneo la Kipawa walilipwa fidia zinazofikia shilingi bilioni 18 ambapo zoezi
hilo lilikamilika Januari 2010.
Katika mwaka
wa Fedha 2010/2011 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 12 za fidia kwa wakazi 864
wa Kigilagila na malipo yalikamilika Januari 2011.
Katika mwaka
2013/14 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 1.2 ikiwa ni fidia kwa wakazi 59 kati
ya wakazi 801 kwa eneo la Kipunguni.
Aidha katika
malipo hayo ni wakazi 742 wa Kipunguni ndio ambao hawajalipwa fidia zao zenye
thamani ya takribani 19.
COMMENTS