MBARAWA ATOA MIEZI 9 KWA MKANDARASI NYAZA ROADS WORKS

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works kukamilisha ujenzi wa barabara ya...



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works kukamilisha ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.
Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kisorya na kusema kuwa usanifu wa barabara na madaraja katika barabara hiyo umewasilishwa sasa ni jukumu la mkandarasi kuendelea na ujenzi kwa kasi na kwa viwango vya ubora.
"Serikali ina nia njema kwa wananchi wa wilaya ya Bunda na mkoa wa Mara sasa tunaijenga barabara hii na mwishon mwa mwaka mtaanza kunufaika nayo", amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo utarahisisha mawasiliano na kupunguza gharama za shughuli za usafirishaji wa samaki, mazao na abiria, uboreshaji makazi na kukuza uchumi kwa maeneo yaliyo kando ya barabara.
Kuhusu suala la fidia, Prof. Mbarawa amefafanua kuwa Serikali italipa fidia kwa mwananchi ambaye barabara imemfuata kama anavyostahili.
"Serikali haina nia ya kumuonea mtu yeyote bali inachofanya inalipa kulingana na sheria inavyoelekeza", amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Makutano-Sanzale KM 50 na kumwagiza mkandarasi wa M/S Mbutu JV Contractor (T) kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kabla ya mwezi Julai mwaka huu.
"Mradi huu ni wa muda mrefu sana na wananchi wameusubiri kwa muda kama hamtamaliza mradi huu mpaka mwezi juni, hii itakuwa kazi yenu ya mwisho, maana ninategemea nyinyi kama wazawa mngekuwa wa mfano" amesisitiza Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema kwa sasa mkoa umeamua kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa miradi ya barabara kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mara, Mhandisi Mlima Ngaile amesema Wakala utasimamia mradi wa ujenzi wa barabara hizo na kuhakikisha mradi unazingatia viwango kulingana na mkataba.
Waziri Prof. Mbarawa yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku mbili akiwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kisorya, wilaya ya Bunda alipokutana nao baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Mara.


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati wa ukaguzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.

Muonekano wa sehemu ya barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.



Muonekano wa sehemu ya barabara ya Makutano-Sanzate yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 54. Barabara hiyo inajengwa na wakandarasi wazawa M/S Mbutu JV.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MBARAWA ATOA MIEZI 9 KWA MKANDARASI NYAZA ROADS WORKS
MBARAWA ATOA MIEZI 9 KWA MKANDARASI NYAZA ROADS WORKS
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimM41u1Yi9duGMiGz0xoaC3Q9s5Uy5uHXPq5QMDvhPyPSz0U9-AyV6_21ZFRo9UoTQuJnzisR_MVXyfT4XfO39pmIUIB3fsrKTVQJdq7yMv5SNxt04FDfzN0iDM2K4Yb9ffd-nOlwB70s/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimM41u1Yi9duGMiGz0xoaC3Q9s5Uy5uHXPq5QMDvhPyPSz0U9-AyV6_21ZFRo9UoTQuJnzisR_MVXyfT4XfO39pmIUIB3fsrKTVQJdq7yMv5SNxt04FDfzN0iDM2K4Yb9ffd-nOlwB70s/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/mbarawa-atoa-miezi-9-kwa-mkandarasi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/mbarawa-atoa-miezi-9-kwa-mkandarasi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy