MADIWANI BUCHOSA WAMKATAA MKURUGENZI

MADIWANI wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na Mkurugenzi wa ...

















MADIWANI wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Cyprian Luanda baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Wametoa ombi hilo (Alhamisi, Februari 15, 2018) katika kikao cha Waziri Mkuu na watumishi Halmashauri ya Buchosa akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.


 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Cyprian Luanda ambaye madiwani wa Halmashauri  hiyo walimwambia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  aondoke nae.

Waziri Mkuu baada ya kupokea ombi hilo alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella kwenda katika halmashauri hiyo na kufanya kikao cha pamoja kati ya Madiwani, Mkurugenzi na watumishi ili kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

Awali, Waziri Mkuu  aliweka jiwe la msingi la hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, ambapo ujenzi wake hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 10.55.

Pia Waziri Mkuu amezindua madarasa manne ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema na kuwata wanafunzi wasome kwa bidii.

Waziri Mkuu amesema wanafunzi hao wanatakiwa wasome sana kwa sababu Rais Dkt. John Magufuli amewaondolea wazazi michango  ya hovyo ili wao wapate fursa ya kusoma.

Pia amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango ili wajikite na masuala ya taaluma. Kama kuna michango kutoka mtu mmoja mmoja, vikundi au Taasisi yote sasa itafikishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri.

Amesema awali wanafunzi walikuwa wanatumika kama njia ya kutengeneza fedha, ambapo wazazi au walezi wanaposhindwa kutoa michango hiyo watoto wao walikuwa wanarudishwa nyumbani. Waziri Mkuu amesema kila mwezi Serikali inapeleka moja kwa moja shuleni sh. bilioni 20.8 kwa ajili ya kugharamia Elimu ya msingi bila malipo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 15, 2018

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MADIWANI BUCHOSA WAMKATAA MKURUGENZI
MADIWANI BUCHOSA WAMKATAA MKURUGENZI
https://i.ytimg.com/vi/tcLn9zlYGXc/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/tcLn9zlYGXc/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/madiwani-buchosa-wamkataa-mkurugenzi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/madiwani-buchosa-wamkataa-mkurugenzi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy