Mbunge wa Ilala Mussa Zungu akieleza changamoto za barabara katika jimbo lake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo. ...
Mbunge wa Ilala Mussa Zungu akieleza changamoto za barabara katika jimbo lake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.

NA K-VIS BLOG
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo ametoa maelekezo kwa watendaji wa Manispaa ya Ilala jijni Dar es salaam kuzuia tabia ya Malori makubwa yenye makontena kuingia katikati jiji kwa kuwa yamekuwa wakisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara zilizojengwa.
Jafo ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara ya kukagua barabara za Manispaa ya Ilala.
Katika ziara hiyo, Jafo ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Zungu ambapo kabla ya kutoa maelekezo hayo wananchi walimlalamikia Waziri Jafo juu ya Malori makubwa kutoka bandarini yanayobeba mizigo ya zaidi ya tani 40 kuingia muda wa usiku na kusababisha uharibifu mkubwa wa barabara hizo zinazojengwa kwa gharama kubwa.
Kwa upande, Mbunge wa Ilala, Zungu amemuomba Waziri Jafo kuliangalia Jimbo la Ilala kwa jicho la pekee kwani barabara zake zina changamoto kubwa sana licha ya kuchangia mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa.
Kutokana na hali hiyo, Jafo ameagiza Manispaa hiyo kuzuia malori hayo ili kuondokana na uharibifu huo.
Kadhalika, Waziri Jafo ametoa maelekezo kwa mratibu wa mradi wa DMDP wa manispaa ya Ilala pamoja na meneja wa TARURA wa Manispaa hiyo kuhakikisha katika mwaka wa fedha 2018/19 barabara za Jimbo hilo zinatengenezwa kwa kiwango cha lami ili kuondoa usumbufu wa madimbwi yanayojaa wakati wa Mvua na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi wa Mchikichini katika ukaguzi wa barabara.

Viongozi wa Ilala wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.
COMMENTS