VYOMBO VYA HABARI VYAHIMIZWA KUWA NA WATUMISHI WA KUTOSHA MKOANI DODOMA
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya Habari Mkoani Dodoma mapema leo. Kulia ni Mkuu wa TBC Kanda ya Kati Bw. Bakari Msulwa.

HomeJamii

VYOMBO VYA HABARI VYAHIMIZWA KUWA NA WATUMISHI WA KUTOSHA MKOANI DODOMA

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbas ametoa wito kwa vyombo vyote vya habari mkoani Dodo...

MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP) WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA
BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA UBUNGO LAPITISHA KWA 100% BAJETI YA ZAIDI YA BILIONI MIA MOJA
SHEREHE YA KUUAGA MWAKA 2016 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2017 PAMOJA NA KUAGA WASTAAFU WA JESHI LA POLISI SHINYANGA


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbas ametoa wito kwa vyombo vyote vya habari mkoani Dodoma na kwingine nchini kuhakikisha wanakuwa na wafanyakazi wa kutosha watakaokidhi mahitaji kutokana na Serikali kuhamia Dodoma.
Dkt. Abbas ametoa wito huo leo mjini Dodoma wakati wa muendelezo wa ziara yake kutembelea vyombo vya habari mkoani humo ambapo leo ametembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Uhuru Redio pamoja na Uhuru gazeti.
“Lengo la ziara yangu ni kuona na kujua changamoto za kiutendaji mnazao kutana nazo pamoja na jinsi gani mmejipanga juu ya ujio wa Serikali kuhamia Dodoma kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani hapa” ameongeza Dkt. Abbas.
Aidha, Dkt. Abbas amevitaka vyombo vya Habari kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano, ubunifu na kufuata maadili katika utendaji kazi hasa katika wakati huu wa mageuzi makubwa nchini.
“Katika mabadiliko au mageuzi yeyote hasa yanayoendelea sasa nchini kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake mahali pake pa kazi ili katika Tanzania ijayo ajivunie si kwa kuwa mlalamishi tu bali ajivunie kuwa naye alishiriki ipasavyo katika safari hii ya mabadiliko” amesisitiza Dkt. Abbas.
Dkt. Abbas ameongeza kuwa “Kwa upande wa habari mimi nimepewa jukumu la kusimamia maadili katika vyombo vya habari hivyo nasimamia na kufuata sheria na busara katika kila jambo linalohusu sekta ya habari ndio maana hatuchukui hatua tu bali tunashauriana na kuonyana kwanza pale wachache wanapokengeuka”.
Mbali na hayo Dkt. Abbas amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anapambana na azma ya kupigania nchi  kujitegemea na si kutegemea nchi za nje kwa maisha yetu yote hivyo vyombo vya habari vinajukumu la kupongeza pale Serikali inapotimiza kazi vyema na kukosoa  pale ambapo Serikali inakosea lakini si kwa kukejeli, kutusi au chombo cha habari kuonekana kinafanya inda.
Ziara hiyo itaendelea kesho mkoani humo ambapo Dkt. Abbas atatembelea vituo vya Redio Alternative Fm (AFm) na Redio Nyemo Fm.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO  na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akikagua vifaa vilivyopo ndani ya moja ya Studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma wakati wa ziara yake mapema leo. (Picha zote na Frank Mvungi- Dodoma)








Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VYOMBO VYA HABARI VYAHIMIZWA KUWA NA WATUMISHI WA KUTOSHA MKOANI DODOMA
VYOMBO VYA HABARI VYAHIMIZWA KUWA NA WATUMISHI WA KUTOSHA MKOANI DODOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRLV6QkuB0ytFF80OCHkI-0wW4xPrCEtSCJPeaJD1aWKY5Dyg7SJXhTxdYEvHMl9DsZu61Wd1Qz9aas71GstHib5hoSqfopNqCatm-TyBRDz-0duJCDEpsLvUAGWxJ9CJHqwcImPYY-q4/s640/1+%25283%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRLV6QkuB0ytFF80OCHkI-0wW4xPrCEtSCJPeaJD1aWKY5Dyg7SJXhTxdYEvHMl9DsZu61Wd1Qz9aas71GstHib5hoSqfopNqCatm-TyBRDz-0duJCDEpsLvUAGWxJ9CJHqwcImPYY-q4/s72-c/1+%25283%2529.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/vyombo-vya-habari-vyahimizwa-kuwa-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/vyombo-vya-habari-vyahimizwa-kuwa-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy