Kamati ya utekelezaji Mkoa wa Kilimanjaro ikiongozwa na Mwenyekiti IVAN SAMSON MOSHI leo tarehe 12/01/2018 imefanya uhakiki wa mal...

Kamati ya utekelezaji Mkoa wa Kilimanjaro ikiongozwa na Mwenyekiti IVAN SAMSON MOSHI leo tarehe 12/01/2018 imefanya uhakiki wa mali za UVCCM KILIMANJARO .
Kamati imebaini mambo mengi ambayo yalitokea kipindi kilichopita na Mwkt ameagiza mikataba yote ipitiwe upya haraka ili kuwezesha UVCCM kunufaika na miradi ya Vijana tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo mambo mengi hayakuwa sawa kwa Vijana!
Baada ya uhakiki ambapo kikao kimechukuwa kutwa nzima wapo wapangaji ambao wameonekana kuwa na mapungufu makubwa katika mikataba yao Mwkt ameunda Kamati ya wajumbe wanne ambao wanafuatilia uhalali wa wao kuwa eneo la Vijana bila taarifa rasmi
Walioteuliwa katika kamati hiyo ni ABDULRAHIM HAMADI Katibu wa Vijana Mkoa Kilimanjaro, YONA MAKWAIA mjumbe kamati ya utekelezaji Mkoa, NICE MUNICY Mjumbe Baraza Kuu Taifa, DICKSON JONATHAN TARIMO Katibu wa UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI MKOA WA
KILIMANJARO, Aidha kamati hiyo ndogo imepewa muda wa siku Tatu kumaliza uchunguzi huo na kuleta taarifa mbele ya Kamati Utekelezaji Mkoa!
IMETOLEWA NA DICKSON TARIMO KATIBU UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI MKOA KILIMANJARO
#KAZIINAENDELEA

COMMENTS