Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda , Leo amehaidi Kuijenga Nyumba ya Vyumba Vinnie (4) Familia ya Mwandishi (mpiga picha) wa M...
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda , Leo amehaidi Kuijenga Nyumba ya Vyumba Vinnie (4) Familia ya Mwandishi (mpiga picha) wa Magazeti ya Serikali TSN wanaochapisha Magazeti ya Habari Leo na Daily News, na SpotLeo, Marehemu Athumani Hamis ambae amezikwa katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Ahadi hiyo Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TSN Dkt. Yonaz kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ambae aliombwa kuisadia familia ya Marehemu ambayo ina watoto Wanne wanaosoma huku wakiwa wanaishia kwenye Nyumba ya kupanga kutokana na Baba yao kuugua kwa zaidi ya Miaka 10 na hivyo kushindwa kufanya kazi.
Dkt. Yonaz amesema Mhe Makonda kwa kutambua mchango wa tasnia ya Habari hususani waandishi wa Habari amekubali kujenga Nyumba hiyo kama kielelezo cha Kumuenzi Marehemu Athumani ambae katika uhai wake alikuwa Mpigapicha mahiri wa Magazeti ya Serikali nchini.
Hatua hii imepokelewa kwa furaha na baadhi ya waandishi wa habari ambao wamesema kitendo cha Makonda kukubali kuijengea nyumba familia ya marehemu Athumani mbali na kuwafuta machozi ya huzuni, bali kimekuwa ni fundisho tosha kwa baadhi ya waandishi ambao walikuwa wakimchukia Mhe Paul Makonda pasipo sababu za msingi, na kukifananisha kitendo hiki na ukamilifu wa maandiko katika vitabu vitakatifu yanayotutaka 'Twapende Adui zetu'
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda (katikati) akizungumza na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSN Ltd Dkt. Jimmy Yonaz kulia na kaka wa Marehemu Athuman Hamis Dkt. Ibrahim Msengi nyumbani kwa marehemu Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam.
COMMENTS