RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA PASIPOTI MPYA YA TANZANIA YA KIELEKTRONIKIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya  ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwa Waziri ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Dkt. Peter Makakala
HomeJamii

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA PASIPOTI MPYA YA TANZANIA YA KIELEKTRONIKIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya  ya kielektronikia baad...

WATANZANIA WAUNGANA NA VIJANA KUTOKA ZAIDI YA NCHI 19 AFRIKA, KATIKA MKUTANO WA MASWALA YA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NAIROBI, KENYA
MASAUNI AFANYA ZIARA NIDA ZANZIBAR, ATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MNAZI MMOJA
RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI









Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2018. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli  akiiangalia  kwa furaha passipoti yake mpya  ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2018. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli  akipokea passipoti yake mpya  ya kielektronikia  kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2018. 

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea pasipoti yake mpya ya kielektronikia kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2018.  


Makamu wa Rais Mhe, Samia Suluhu Hassan akionesha passipot yake ya kielekroniki baaya kukabidhiwa wakati wa uzinduzi huo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sahihi kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya  makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sahihi kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya  makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli  akiwa na  Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakisubiri hatua inayofuata  baada ya kuweka sahihi kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya ya kielektronikia makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sahihi kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya  makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.  


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akichukuliwa alama za vidole kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya ya kielektronikia makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.  


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Mwigulu Nchemba wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Dkt. Peter Makakala akielezea hatua mbalimbali za upatikanaji wa passipoti mpya  ya Tanzania ya kielektronikia makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.
  


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  akichukuliiwa alama za vidole  kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya ya kielektronikia  makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2018.  



Sehemu ya Maafisa waandamizi wa Uhamiaji wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa kwenye sherehe za uzinduzi wa  pasipoti  mpya ya Tanzania kielektronikia  makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2018.  (PICHA NA IKULU)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Januari, 2018 amezindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.
Uzinduzi wa mfumo huo umefanyika katika ofisi kuu ya uhamiaji Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Seif Ali Iddi, na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Wengine ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume.
Kabla ya kuzindua mfumo wa uhamiaji mtandao Mhe. Rais Magufuli amekagua teknolojia iliyotumika katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa alama za vidole na baadaye kupatiwa pasipoti mpya ya kielekektronikia (e-Passport) ambayo pia imeanza kutolewa leo.
Pasipoti mpya za kielektronikia pia zimetolewa kwa viongozi wengine wakuu wa Serikali, Bunge na Mahakama wa Tanzania Bara na Zanzibar, waliohudhuria uzinduzi huo.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Idara ya Uhamiaji kwa kufanikisha mradi wa kuweka mfumo wa uhamiaji mtandao na kuanza kutoa pasipoti mpya ya kielektronikia kwa gharama nafuu ya Shilingi Bilioni 127.2 ikilinganishwa na makadirio yaliyowekwa awali ya Shilingi Bilioni 400.
“Hapa tumeokoa fedha nyingi za Watanzania, kuna watu walikuwa wamejiandaa kutupiga na kuchukua hizo Shilingi Bilioni 400, lakini tukatumia vyombo vyetu mbalimbali, tukafanya uchunguzi na tumefanikiwa kutekeleza mradi huu kwa gharama nafuu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na idara ya uhamiaji baada ya kupokea maelekezo yake ya kutakiwa kufanya mabadiliko makubwa, Mhe. Rais Magufuli ameahidi kutoa Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kujenga ofisi ya makao makuu ya idara hiyo Mjini Dodoma.
“Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala na timu yako mnafanya kazi nzuri, ndio maana nimewanunulia nyumba 103 kwa ajili ya wafanyakazi kule Dodoma na leo nitawapa fedha nyingine Shilingi Bilioni 10 mkajenge ofisi nzuri ya makao makuu, nyinyi endeleeni kuchapa kazi, endeleeni kukamata wahamiaji haramu na endeleeni kukusanya mapato vizuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mapema akitoa taarifa ya mfumo wa uhamiaji mtandao, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amesema mfumo huo ni muunganiko wa mifumo mbalimbali ambayo imesanifiwa kufanya kazi kwa pamoja, kutoa taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za kiuhamiaji na kwamba kupitia mfumo huo idara ya uhamiaji inatarajia kutoa pasipoti za kielektronikia (e-Passport), viza za kielektronikia (e-Visa), vibali vya ukaazi vya kielektronikia (e-Permit) na udhibiti wa mipaka wa kielektronikia (e-Border Management) kwa awamu nne hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu 2018, pamoja na kutoa pasipoti ya kielektronikia ya Afrika Mashariki ya Tanzania.
Balozi wa Ireland hapa nchini Mhe. Paul Sherlock ameipongeza Tanzania kwa kufanikisha mradi huu na kueleza kuwa mfumo huu wa uhamiaji mtandao ni alama muhimu ya Taifa.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

31 Januari, 2018







Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA PASIPOTI MPYA YA TANZANIA YA KIELEKTRONIKIA
RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA PASIPOTI MPYA YA TANZANIA YA KIELEKTRONIKIA
https://i.ytimg.com/vi/GhnTUWX5iPg/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/GhnTUWX5iPg/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/rais-dkt-magufuli-azindua-pasipoti-mpya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/rais-dkt-magufuli-azindua-pasipoti-mpya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy