NEC YATOA TAARIFA UCHAGUZI MDOGO WA MWEZI FEBRUARI
HomeSiasa

NEC YATOA TAARIFA UCHAGUZI MDOGO WA MWEZI FEBRUARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetanga...

MANGULA AZUNGUMZA NA WENYEVITI WA MASHINA KINONDONI, ASEMA WASALITI WALIWABEBA WAPINZANI DAR
SHAKA AZUNGUMZIA MAENDELEO YA UCHAGUZI WA NDANI WA UVCCM
MBUNGE MAJI MAREFU AWA GUMZO ASHIRIKI KUFYATUA MATOFALI BAADA YA KUFUNGUA KIWANDA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
nembo%20ya%20NEC

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nyingine sita utafanyika Februari 17 mwaka huu.

Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage alisema jana kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalibali zikiwemo kifo na baadhi ya madiwani kujiuzulu.

Alizitaja kata ambazo zitafanya uchaguzi huo mdogo kuwa ni Kata ya Buhangaza iliyoko katika Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Kata ya Kanyelele iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kata ya Mitunduruni iliyoko katika Manispaa ya Singida.

Kata zingine ambazo zitafanya uchaguzi ni kata ya Kashashi, Gararagua na Donyomuruak ambazo madiwani wake wamejiuzulu hivi karibuni.

“Napenda kutumia nafasi hii kutoa tarifa kwa umma kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hizo februari 17, 2018,”alisema Jaji Kaijage.

Uchaguzi huo unafanyika sambamba na uchaguzi mwingine mdogo wa wabunge ambao utafanyika katika majimbo mawili ya Songea Mjini ambako mbunge alifariki na Longido mbunge wake alivuliwa ubunge na mahakama.

Aliongeza kuwa kutokana na uchaguzi huo mdogo, ratiba ya uchaguzi huo itaanza tarehe 18 hadi 24 Januari ambako tume itatoa fumu za uteuzi, uteuzi wa wagombea utafanyika januari 24 na kampeni zitaanza Januari 25 hadi Februari 16 na uchaguzi wenyewe utafanyika Febuari 17.

Kaijage alitoa mwito kwa vyama vya siasa, wadau wa uchaguzi na wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo.

“Tume inaviasa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya katiba, sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa, kanuni za uchaguzi na serikiali za mtiaa za mwaka 2015, maadili ya uchaguzi pamoja na maelekezo yaliyotolewa na tume katika kipindi chote cha uchaguzi mdogo,”alisema Jaji Kaijange.



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NEC YATOA TAARIFA UCHAGUZI MDOGO WA MWEZI FEBRUARI
NEC YATOA TAARIFA UCHAGUZI MDOGO WA MWEZI FEBRUARI
https://lh5.googleusercontent.com/cQIGm29Ul5V5LE1D6X-WC6Go86oCHJwobxk4x3lvcdBGOgX-pTkRotweWQqnZOhTsnnI8U-Oq2qOw80MxshsxCIeaQ84XAsJdFyNQNHN1ZjDgzuKUbniTgvudrf6ChPuzhscxuFMrhgpBjVZbA
https://lh5.googleusercontent.com/cQIGm29Ul5V5LE1D6X-WC6Go86oCHJwobxk4x3lvcdBGOgX-pTkRotweWQqnZOhTsnnI8U-Oq2qOw80MxshsxCIeaQ84XAsJdFyNQNHN1ZjDgzuKUbniTgvudrf6ChPuzhscxuFMrhgpBjVZbA=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/nec-yatoa-taarifa-uchaguzi-mdogo-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/nec-yatoa-taarifa-uchaguzi-mdogo-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy