MANGULA AZUNGUMZA NA WENYEVITI WA MASHINA KINONDONI, ASEMA WASALITI WALIWABEBA WAPINZANI DAR
HomeSiasa

MANGULA AZUNGUMZA NA WENYEVITI WA MASHINA KINONDONI, ASEMA WASALITI WALIWABEBA WAPINZANI DAR

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Philip Mangula akizungumza na Wenyeviti wapya wa Mashina ya CCM waliochaguliwa katik...


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Philip Mangula akizungumza na Wenyeviti wapya wa Mashina ya CCM waliochaguliwa katika uchaguzi ndani ya Chama, uliofanyika hivi karibuni, alipokutana nao leo katika Ukumbi wa Vijana Sodial Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 

------------------

Na Bashir Nkoromo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara Philip  Mangula, amesema wapinzani hawakuwa na uwezo wa kushinda katika baadhi ya majimbo na kata  jijini Dar es Salaam, katika uchaguzi mkuu uliopita isipokuwa walisaidiwa na wasaliti ndani ya chama.

Amesema, kutokana na madhara hayo, CCM itaendelea kuwasaka na kuwang'oa wasaliti hao, wakiwemo wale waliofanikiwa kujipenyeza na kushinda nafasi mbalimbali katika uchaguzi ndani ya Chama CCM na ndiyo maana CCM imefuta uchaguzi kwenye baadhi ya kata.

Mangula amesema hayo leo katika kikao chake na Wenyeviti wapya wa Mashina ya CCM, kutoka kata za Kawe na Kinondoni, waliochaguliwa hivi karibuni, kilichofanyika leo Vijana Social Hall, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema, tayari chama kimeshachukua hatua mbalimbali kwa wasaliti kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na kata kwa kuwapa adhabu zikiwemo za kuwafuta uanachama, onyo kali na wengine kuendelea kuchunguzwa.

"japokuwa tumekwishachukua hatua mbalimbali dhidi ya wasaliti lakini bado kazi hii inaendelea hadi tuhakikishe tabia hii chafu ya usaliti inakoma ndani ya chama, kwa sababu ni jambo la kushangaza CCM yenye wanachama wengi kiasi hiki kuliko chama chochote inapoteza majimbo katika mazingira yasiyo na majibu", alisema Mangula.

Akitoa tathimini kuhusiana na wasaliti ngazi ya mkoa, alisema jumla ya viongozi 4595 walikuwa wasaliti ndani ya Chama walipewa onyo, huku 3907 wapo chini ya uangalizi wa miezi 12.

Wengine waliopewa kalipio ya miezi 18 walikuwa 4, wengine 398 wapo katika uchunguzi, 465 wameadhibiwa, huku waliofukuzwa na kuvuliwa uwanachama wapo 2267.

Mangula aliwataka Wenyeviti hao wapya kuwa mstari wa mbele kuhakikisha CCM inaimarika katika maeneo yao kwa kuzingatia misingi na kanuni ambayo mojawapo ni kuepuka kupokea na kutoa rushwa hasa nyakati za uchaguzi.

Akimkaribisha mangula kuzungumza na wenyeviti hao, katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe aliwataka watendaji katika matawi yenye miradi kuisimamia kwa makini midari hiyo hasa upande wa mapato, ili mapato yanayopatikana yatumike pia kuwalipa japo kidogo wenyeviti wa mashina.


 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akiwasili katika ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni Dar es Salaam, kuzungumza na Wenyeviti wa Mashina kutoka Kata za Kawe na Kinondoni, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe.

 Wenyeviti wa CCM wa matawi wakimshangilia Mangula alipoingia ukumbini

 Mangula akiwa meza kuu baada ya kuwasili ukumbini 

 Wenyeviti hao wakishangilia ukumbini

 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula, kuzungumza na wenyeviti hao wa mashina

 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara Philip Mangula akizungumza na Wenyeviti hao wa mashina kutoka katika Kata za Kawe na Kinondoni, Dar es Salaam, leo

 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara Philip Mangula akikabidhi vitendea kazi kwa mwenyekiti wa shina namba 12 Oysterbay, James Nyakyoka, alipokabidhi vifaa hivyo kwa wenyeviti hao baada ya kuzungumza nao leo. (PICHA BASHIR NKOROMO)

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MANGULA AZUNGUMZA NA WENYEVITI WA MASHINA KINONDONI, ASEMA WASALITI WALIWABEBA WAPINZANI DAR
MANGULA AZUNGUMZA NA WENYEVITI WA MASHINA KINONDONI, ASEMA WASALITI WALIWABEBA WAPINZANI DAR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiA5F2tCoB8WuhA1XqTEJpqfNS3EE14N0uK_piYMDidE_G6GtuWNgWHhpgPaE3K_od6nPel3_2aGKk131lzTGykdpt6SkRxDnXK9V5MnzLuq-tTZlVrbq8fG_IFPPUyWqxwWLqxl0dYbiAI/s400/1.+BN648428.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiA5F2tCoB8WuhA1XqTEJpqfNS3EE14N0uK_piYMDidE_G6GtuWNgWHhpgPaE3K_od6nPel3_2aGKk131lzTGykdpt6SkRxDnXK9V5MnzLuq-tTZlVrbq8fG_IFPPUyWqxwWLqxl0dYbiAI/s72-c/1.+BN648428.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/mangula-azungumza-na-wenyeviti-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/mangula-azungumza-na-wenyeviti-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy