NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (pichani juu na chini) ameongoza zoezi la kuteketeza nyavu (ndogo), 242 zenye thamani...

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (pichani juu na chini) ameongoza zoezi la kuteketeza nyavu (ndogo), 242 zenye thamani ya sh milioni 242 baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe.
Hatua hiyo minafuatia agizo la serikali, kuwataka wavuvi katika kisiwa cha Zilagula halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema kusalimisha nyavu hizo kwa hoiari kabla mkono wa sheria haujawafikia.
Kwa mujibu wa Mhe., Naibu Waziri, “uvuvi haramu unakuwa tishio kwa rasilimali zetu ambapo kulingana na utafiti inaonyesha samaki wazazi walikuwa wamebaki asilimia 4 wakati wachanga wapo asilimia 93”. Alisema.
Alisema kama uvuvi haramu hautakomeshwa utasababisha ziwa kuwa jangwa na kuwaagiza viongozi wa serikali wa eneo husika kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha wanalinda rasilimali kwa kuzuia uvuvi haramu.





COMMENTS