Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Dkt.Delila ...
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Dkt.Delila Kimambo(kulia), akimwelezajambo Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, maendeleo ya afya za mapacha walioungana, Maria na Consolata, waliolazwa kwenye Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu.Katika hatua nyingine Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust Fund (TTF), ametoa TV sita kwa JKCI ambazo zimefungwa katika wodi na kliniki za watoto.

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwajulia hali pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Fedha Agnes Kuhenga Televisheni moja kati ya nne zilizotolewa na Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Jumla ya TV sita zimetolewa na Tulia Trust ambazo zimefungwa katika wodi na kliniki za watoto.

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu. Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust Fund (TTF), ametoa TV sita kwa JKCI ambazo zimefungwa katika wodi na kliniki za watoto.

Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu. (PICHA NA JKCI)
COMMENTS