KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI DKT. MASHINGO AWATAKA WAFUGAJI KUHAKIKISHA IFIKAPO JANUARI 31 MIFUGO YOTE NCHINI IWE IMEPIGWA CHAPA
HomeJamii

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI DKT. MASHINGO AWATAKA WAFUGAJI KUHAKIKISHA IFIKAPO JANUARI 31 MIFUGO YOTE NCHINI IWE IMEPIGWA CHAPA

 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa...

TANZANIA NA INDIA KUDUMISHA USHIRIKIANO MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN
WAFANYAKAZI WA VODACOM-TANZANIA WAPIMA AFYA ZAO
UN YAADHIMISHA MIAKA 71, YAAHIDI KUWEZESHA VIJANA

 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo
akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa
Katavi leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji
kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria
Mashingo akiwaonesha wafugaji sehemu sahihi ambayo ng’ombe anatakiwa kupigwa
chapa ili kuepuka kuiraribu ngozi baada ya kushiriki zoezi la upigaji chapa
katika Kijiji cha Igalula wilayani Tanganyika mkoani Katavi leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo
akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa
Katavi mapema leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji
kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
Na Kumbuka Ndatta, WMUV



KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)
Dk. Maria Mashingo amewataka wafugaji kuhakikisha wamekamilisha zoezi la upigaji
chapa mifugo yao kabla ya muda ulioongezwa na Serikali wa hadi Januari 31 mwaka
huu kwani baada muda huo kupita haijulikani Serikali itaamua nini kuhusu mifugo
itakayokuwa haijapigwa chapa.



Akizungumza
wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Igalula Kata
ya Mpanda ndogo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Dk. Mashingo alisema zoezi
hilo la upigaji chapa  linatekelezwa kwa
mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na  ufuatiliaji wa mifugo  
Na. 12 ya Mwaka 2010 .



Dk. Mashingo alisema upigaji
chapa umelenga kudhibiti magonjwa ya mifugo,wizi wa mifugo, uimarishaji  usalama wa afya na mazao ya mifugo sambamba na
kudhibiti usafirishaji na uhamaji wa mifugo kiholela na kuimarisha biashara ya
mifugo na mazao yake kitaifa na kimataifa.


"Wafugaji hakikisheni mifugo yenu yote
inapigwa chapa kwani baada ya Januari 31 mwaka huu hatujui Serikali itaamua
nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa "alisema.



Dk. Mashingo alisema pamoja nia njema ya
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwatetea wafugaji wanaofanyiwa vitendo vya uonevu na
mamlaka nyingine za Serikali pia aliwahimiza kutii sheria za nchi kwa
kutoingiza mifugo yao kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.



Pia aliwakumbusha wafugaji kutambua kuwa
rasilimali ya mifugo waliyonayo ina thamani kubwa na kwamba wao pia ni sehemu
ya wawekezaji  hivyo ni vyema wakatengeza
miundombinu bora kwa ajili ya mifugo yao kuliko kuisubiri Serikali pekee kujenga
miundombinu hiyo.



“Wafugaji ni wawekezaji muhimu sana katika
nchi yetu kwani kama wasingekuwepo nchi ingelazimika kuagiza mazao ya mifugo
kutoka nje ya nchi na tungelazmika kutumia sh. trioni 17 kwa mwaka”alisema  Dk. Mashingo.



Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Cresencia
Joseph amemweleza Dk. Mashingo kuwa mkoa huo
unajumla ya ng'ombe 570,758  ambapo
kati ya hao 423,767 wameshapigwa chapa.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI DKT. MASHINGO AWATAKA WAFUGAJI KUHAKIKISHA IFIKAPO JANUARI 31 MIFUGO YOTE NCHINI IWE IMEPIGWA CHAPA
KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI DKT. MASHINGO AWATAKA WAFUGAJI KUHAKIKISHA IFIKAPO JANUARI 31 MIFUGO YOTE NCHINI IWE IMEPIGWA CHAPA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPzVBnxudk9TNbgozgEIYwA2xWgkjQvOXGjRH_PmXoIPpZxznUtfSOPgnk4ya_nJh8-jGt2ngYIUVnTs7r4Z5RVk4MOcgP4tSH0b18CVniKj8KVtUF4r3PnTd7GsdbFMo51BZF3auV-cdi/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPzVBnxudk9TNbgozgEIYwA2xWgkjQvOXGjRH_PmXoIPpZxznUtfSOPgnk4ya_nJh8-jGt2ngYIUVnTs7r4Z5RVk4MOcgP4tSH0b18CVniKj8KVtUF4r3PnTd7GsdbFMo51BZF3auV-cdi/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/katibu-mkuu-wizara-ya-mifugo-na-uvuvi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/katibu-mkuu-wizara-ya-mifugo-na-uvuvi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy