CCM WILAYA YA GEITA WALAANI JESHI LA ZIMA MOTO KUWATOZA FEDHA KUBWA WACHIMBAJI BILA YA KUWAPATIA RISITI

Baadhi ya wachimbaji wa kijiji na kata ya Rwamgasa wakiendelea na kazi ya uchanjuaji wa madini ya dhahabu. Moja kati ya wamiliki wa mialo ya...







Baadhi ya wachimbaji wa kijiji na kata ya Rwamgasa wakiendelea na kazi ya uchanjuaji wa madini ya dhahabu.



Moja kati ya wamiliki wa mialo ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu akionesha risti ambayo sio ya EFD ambayo wamekuwa wakipatiwa baada ya kununua kifaa cha kuzimia moto.



Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi(CCM)Wilayani Geita Jonathan Masele akizungumza na wachimbaji baada ya kufika kwenye maeneo yao ya kazi na kukutwa baadhi ya makarasha yamefungwa na Jeshi la Zima moto na uokoaji.



Eneo la kuchenjulia dhahabu likiwa limefungwa na jeshi la zima moto na uokoaji.





Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Barnabas Mapande akikagua moja kati ya mtungi wa kuzimia moto wakati alipofika kuzungumza na kusikiliza changamoto za wachimbaji.





Kifaa cha kuzimia moto kikiwa kwenye eneo la kuchenjulia dhahabu.


Na,Joel Maduka,Geita.
Chama cha mapinduzi Wilayani Geita kimelaani kitendo cha jeshi la zima moto na uokoaji kuwatoza gharama kubwa bila ya kuwapa stakabadhi za serikali baadhi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye kijiji cha Lwamgasa huku wakifungiwa shughuli za uchenjuaji madini hayo kutokana na baadhi yao kugoma kununua kifaa cha kuzimia moto.


Akizungumza baada ya kufika kwenye machimbo hayo na kujionea namna ambavyo wachimbaji hao wamefungiwa shughuli zao Katibu Mwenezi wa CCM Wilayani Humo Bw Jonatham Masele,amesema CCM imesikitishwa na jeshi la zima moto kuwatoza Sh Lakini moja na elfu ishirini.


“Kiukweli sisi kama chama tumesikitishwa sanaa na kitendo cha jeshi la zima moto kuuza kwa bei kubwa bila ya kutoa risti mitungi hii ya gesi ya kuzimia moto na jambo jingine kuwafungia watu shughuli zao bila ya kuwapa elimu jambo hili sio nzuri tunaomba wajitahidi kuwaelimisha kwanza awa watu nasio kujichukulia hatua ya kuwafungia”Alisema Masele.


Bw Lehamu Lugiko , Mzee Mathew Kajoro na Mwananyanzara Hamis wameelezea sababu kubwa ambayo imeendelea kuwapa mashaka wachimbaji kuwa ni kuuziwa mitungi ya kuzimia moto bila ya kupewa Elimu ambayo itawasaidia kupambana na majanga ya moto huku wakisikitishwa na kitendo cha kufungiwa kwa shughuli zao.


Mkuu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Geita Bw Elisa Mgisha amesema wao sio wasambazaji kwani kuna watu ambao ni mawakala na kwamba suala la risti za EFD inatokana na wafanyabiashara wenyewe na kuhusu kuuziwa kwa bei kubwa ni kwamba wao wanapotoa kibari cha mawakala yeye ndiye mwenye jukumu la kupanga bei ya kuuza mtungi vile ambavyo anaonelea.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Bw Barnabas Mapande amemtaka mkuu wa jeshi la zima moto kushughulikia tatizo hilo na kuacha kuendelea kuwakandamiza wananchi na wafanyabiashara pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao za kujitafutia kipato.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: CCM WILAYA YA GEITA WALAANI JESHI LA ZIMA MOTO KUWATOZA FEDHA KUBWA WACHIMBAJI BILA YA KUWAPATIA RISITI
CCM WILAYA YA GEITA WALAANI JESHI LA ZIMA MOTO KUWATOZA FEDHA KUBWA WACHIMBAJI BILA YA KUWAPATIA RISITI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDL_Tzt-D1iqfG1qQrkmw-bUiEFTldG2pjJMdx_G3-mWuBciIeRuqIcnBqlKiK176tmGRs7cs1B7ms0dwxUSoA601OCk45oGNyJMvtqzJaLAh1U3x_sCS2VWQ_Y6d7WBo7xIg3HjcCu6o/s640/DSC_0135.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDL_Tzt-D1iqfG1qQrkmw-bUiEFTldG2pjJMdx_G3-mWuBciIeRuqIcnBqlKiK176tmGRs7cs1B7ms0dwxUSoA601OCk45oGNyJMvtqzJaLAh1U3x_sCS2VWQ_Y6d7WBo7xIg3HjcCu6o/s72-c/DSC_0135.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/ccm-wilaya-ya-geita-walaani-jeshi-la.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/ccm-wilaya-ya-geita-walaani-jeshi-la.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy