Mchungaji Tito (pichanijuu), ambaye kwa takriban wiki nzima ameibua mjadala mkubwa mionhgoni mwa Watanzania, kufuatia vi...

Mchungaji Tito (pichanijuu), ambaye kwa takriban wiki nzima ameibua mjadala mkubwa mionhgoni mwa Watanzania, kufuatia video inayomuonyesha akiwa na wanawake wawili mmoja akimtambulisha kuwa mkewe na mwingine msichana wa kazi (house girl) huku akiwapiga busu amekamatwa leo Januari 23, 2018 mkoani Dodoma.
Awali Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Marlin Komba amesema hamtambui mtu anayejiita nabii Tito na kwamba hajasajili kanisa lake katika ofisi ya msajili wa taasisi za dini, na kwamba Serikali imeona vitendo anavyovifanya ‘nabii’ huyo kupitia mitandao ya kijamii na imeanza kuchukua hatua.“Ninachoweza kusema ni kwamba hakuna mtu anayezuiwa kuongea hapa nchini, mwache aongee anavyoweza ila Serikali imeshaona anachokifanya na yanayoendelea mitandaoni hatua zinachukuliwa dhidi yake,” amesema Komba.Kauli hii imekuja kufuatia kusambaa kwa video mbalimbali zikimuonyesha ‘nabii’ huyo akitoa mafundisho yake huku akinywa vilevi pamoja na kufanya matendo ambayo ni kinyume cha maadili ya dini, jambo ambalo limeonekana kuwakera wadau wengi wa dini.Kwa upande wao viongozi mbalimbali wa dini wameonyeshwa kukerwa na kulaani vitendo anavyovifanya mtu huyo anayejiita ‘nabii’ na kusisitiza kuwa hakuna dini inayoruhusu hayo.Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza amesema kuwa, kutokana na vitendo anavyofanya, mtu huyo hapaswi kujiita mtumishi wa Mungu.“Huyo hawezi kuwa mtumishi wa Mungu na wala hafanyi huduma ya kanisa. Ni vyema watu kama hawa wafuatiliwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Natumaini Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndani yake ina ofisi ya msajili wa taasisi za dini itafanya kazi yake,” amesema Mchungaji Lwiza.Naye Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Rajab Katimba amesisitiza Serikali na viongozi wa dini kuingilia kati suala hilo na kueleza kuwa, hakuna kitabu chochote cha dini kinachohamasisha ulevi na ukosefu wa maadili.“Hilo suala linakwenda tofauti na dini na mila na desturi zetu pia. Dini zinatakiwa kuleta amani na kuhamasisha watu waheshimiane si kuzungumza mambo yanayokiuka maadili yetu. Naona ipo haja ya viongozi wa dini na Serikali kuingilia suala hili na waende mbali zaidi kwa kuongea naye huenda hafahamu anachokifanya,” amesema Rajab Katimba.
ALIYEJIHITA NABII "MTATA" MIKONONI MWA POLISI HUKO DODOMA
Labels:
Jamii 3473
Advertisement

MAIN QUOTE
x cbfgmfg hghg
- Steve Jobs
WEEK TRENDING
Loading...
YEAR POPULAR
HUYU NDIYE MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI MWANAMA Mikel Ruffinelli mkazi wa Los Angeles, Marekani, amedhihirisha k...
Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha Meja Jenerali Paul Mssao akitoa taarifa ya maofisa wapya kwa Amiri ...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza...
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kufunga mafunzo ya ...
Msomaji wa Quran tukufu katika mashindano ya kitaifa, Abdallah Abdulkadri akisoma wakati wa fainali zake mashindano Dar es Sal...
COMMENTS